The House of Favourite Newspapers

 Wakali 30 kuweka historia  Dar Live Mei 21

0

WAKALI thelathini kutoka katika vikundi vya Muziki wa Taarab wakiongozwa na Mzee Yusuf, Patricia Hilary na Khadija Kopa wanatarajia kuweka historia jukwaa la Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar, Mei 21, mwaka huu.

Akizungumza na Showbiz Extra, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo aliwataja wakali hao watakaoweka historia kwa mara ya kwanza tangu kuwepo kwa muziki wa Taarab nchini kuwa ni Leila Rashid, Hadija Yusuf, Bi Mwanahawa, Joha Kassim kutoka Jahazi Modern, Hadija Kopa, Otham Sudi, Mwanaidi Shaban kutoka Muungano, Shakira kutoka J.K.T, Misambano na Kisauji kutoka Babloom na wengine kibao.

“Utakuwa ni usiku wa kukumbukwa na kila mmoja kwa maana kuwa itakuwa ni mara ya kwanza kwa vikundi hivyo kukutana katika jukwaa la Dar Live,” alisema Mbizo.

Wakali wengine wanaotarajiwa kuwepo ni Sabaha Mchacho, Sihaba Juma, Hassan Soud, Thabit Abdul, Sizya Mazongela, Mustafa, Zubeda Mlamali na wengine kibao.

Leave A Reply