Rayvanny, Juma Nature, Mzee wa Bwax, Young Killer Kukinukisha Dar Live

MAMBO ni mengi lakini muda nao ni mchache! Listi inazidi kumwagika kuelekea Vanny Day ndani ya Idd Pili katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar ambapo sasa wakali kibao wanatarajiwa kuliamsha.

 

Akizungumza na Risasi Vibes, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ ambaye siku hiyo ataisimamisha Dar kwa masaa kadhaa alisema kuwa, utakuwa ni usiku wa kihistoria tangu aanze muziki kwani hajawahi kabisa kutumia kiwanja hicho cha burudani hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia.

 

“Nitapiga live kwa kutumia vyombo nyimbo zangu zote zaidi ya 25 ndani ya Dar Live na huenda nikafungua shoo mapema sana tofauti na wasanii wengine wanavyofanya. Kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi,” alisema Rayvanny na kuongeza baadhi ya listi ya wakali watakaoliamsha.

 

“Tutakuwa pia na Juma Nature, Mzee wa Bwax, Young Killer pamoja na Gigy Money. Ujue listi ni ndefu sana na mashabiki wategemee sapraiz nyingi na kubwa sana,” alimaliza Rayvanny. Kujua kiingilio, endelea kufuatilia Magazeti ya Global Publishers.

Risasi Vibes


Loading...

Toa comment