The House of Favourite Newspapers

WAKALI WA ASISTI AFRIKA

Emmanuel Okwi

HATA uzungumze kwa lugha gani ya kejeli unayoijua wewe, ukweli unabaki palepale Simba ni miongoni mwa klabu nane bora za Afrika msimu huu. Yaani hakuna cha Asec Memosas, Orlando Pirates sijui Ismailia, wote hao wanasubiri kwa Simba ya Mohammed Dewji ‘Mo’.

 

Klabu nyingi kitakwimu na kimiundombinu zinaweza zikaizidi Simba lakini mwisho wa siku soka ni matokeo ya uwanjani. Simba imecheza karata zake ndani na nje ya uwanja na sasa imetinga kwenye hatua ya klabu nane za soka za Afrika kwa msimu wa 2018/19.

 

Ni hatua kubwa ambayo Simba imepiga msimu huu. Lakini kwa mujibu wa CAF ambayo ndiyo waratibu wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kwenye hatua ya makundi Simba imeingiza wachezaji wawili kwenye orodha ya asisti. Ameingia mkali Emmanuel Okwi na mzee wa vichwa, John Bocco, hebu angalia chati yao;

`

LIGI YA MABINGWA ASISTI 4

 

Kwenye hatua ya nane bora ya Ligi ya Mabingwa kuna wakali wawili wazoefu halafu kina Okwi wanafuata. Tresor Mputu Mabi wa TP Mazembe na Gaston Sirino wa Mamelodi Sundowns kila mmoja ana asisti nne. Ni wachezaji muhimu sana kwenye klabu zao na wenye uzoefu na michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu Afrika.

 

ASISTI 3

Hussein El Shahat wa Al Ahly SC na yule jamaa msumbufu wa Mazembe, Jackson Muleka wote wana tatu. Pengine ni kutokana na ugumu wa hatua hiyo lakini wamefanya kazi kubwa kuzibeba klabu zao na mashabiki wao walidhani walipaswa kuwa na asisti nyingi kuliko hizo.

 

ASISTI 2 Hapa kuna wanetu wawili. Emmanuel Okwi na John Bocco. Ni Wachezaji ambao wameifanya kazi yao vizuri tangu hatua za awali ambazo Simba imeanza mashindano ya msimu huu.

 

Anapokosekana mmoja wao pengo linaonekana. Wote wana asisti mbili kama Glody Ngonda wa AS Vita na Mohamed Hany wa Al Ahly ile iliyokula moja Taifa.

Abdenour Belkheir wa CS Constantine ile timu bishi kufungika na Ismail El Haddad wa Wydad AC nao wana asisti mbili. Wengine ni Tuisila Kisinda wa AS Vita, Youcef Belaili wa Esperance Tunis Houcine Benayada wa CS Constantine na Ali Maaloul wa Al Ahly.

 

MTAA WA PILI Kwenye Kombe la Shirikisho pia kulikuwa na wakali hawa wa Asisti hatua ya makundi. Aliyekuwa na asisti nne ni Abdelilah Hafidi wa Raja CA. Jacques Tuyisenge wa Gormahia yule ambaye Simba walikuwa wanamtaka ana asisti mbili na timu yake imefuzu robo fainali. Wengine wenye mbili ni Songné Yacouba wa Asante Kotoko,Tiago

 

BOCCO Ni Kapteni ambaye amekuwa na mchango mkubwa ndani ya Simba msimu huu
SIRINO Wasauzi wanamuelewa sana haswa mashabiki wa Mamelody na amewabeba sana msimu huu mpaka walipofikia

Azulao wa Petro Atletico,Abdallah Gomaa wa Zamalek SC. Wengine ni Walter Bwalya wa Nkana FC, Kodjo Fo Doh Laba wa RS Berkane, Mehdi Oubilla wa Hassania Agadir na Idris Mbombo wa Al Hilal Omdurman

Comments are closed.