The House of Favourite Newspapers

WAKATI AKITIMIZA MIAKA 10 SKENDO YA FREEMASON YAZIDI KUMTESA MONDI

DAR ES SALAAM: Wakati akitimiza miaka kumi ya ustaa wake ndani ya Bongo Fleva, mwanamuziki mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amezidi kugandwa na skendo ya Freemason na hivyo kuzidi kmtesa msanii huyo, Amani limedokezwa.  Chanzo cha karibu na Diamond kimedai kuwa kuhusishwa huko na mambo ya Freemason kumekuwa kukimhuzunisha msanii huyo ambaye anaamini mafanikio yake yanatoka na yeye kujituma katika kazi.

“Diamond anapenda watu wathamini kazi zake kama sehemu ya jitihada anazofanya yeye na viongozi wake, hataki mafanikio yake yapimwe kama yanakuja kirahisi kwa nguvu za giza,” chanzo kilisema. Madai mapya juu ya Diamond au Mondi na Freemason yamesambaa hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii kwamba jamaa huyo ni gwiji wa makafara ya damu yanayomfanya kuwa juu kimuziki, kukusanya umati mkubwa kwenye shoo zake na kuwa na utajiri mkubwa.

MONDI NA FREEMASON

Madai dhidi ya Mondi kuhusishwa na Freemason yamekuwepo tangu mwaka 2013, lakini yanaonekana kuibuka upya baada ya jamaa huyo kuendelea kupasua anga pamoja na kwamba yalitabiriwa mengi hasa juu ya anguko lake.

Kufuatia mafanikio ya Mondi, madai ya mtandaoni ni kwamba, staa huyo amepata mafanikio ya harakaharaka kwa msaada wa Freemason jamii ya siri inayodaiwa kuwawezesha watu kupata utajiri na umaarufu kwa ghafla.

Inadaiwa kuwa, mbali na kufunika kwa shoo zake na kujaza viwanja vya mpira ndani na nje ya Bongo, utajiri wa ghafla na nyota kali aliyonayo, lakini pia Freemason wanahusika na kung’arisha nyota yake na kumfanya kukubalika ile mbaya ndani na nje ya Bongo. Katika shoo zake kibao, Mondi ameendelea kutikisa na ‘kuteka’ miji na nchi mbalimbali.

MAVAZI

Kwa mujibu wa madai ya mitandaoni, Mondi amekuwa akivaa mavazi, cheni na pete zenye nembo zinazodaiwa kuwa za Freemason kama sehemu ya masharti ya kuwa mwanachama wake huku akiweka ishara zao kila anapopiga picha.

NEMBO ZA FREEMASON

“Kinachomponza ni mavazi yake, cheni na pete zenye nembo za Freemason ambazo zinadaiwa ndizo zinamfanya ang’are popote anapokuwa. “Ukiacha mavazi kuna ishara mbalimbali ambazo zinaaminika hutumiwa na Freemason katika kuwasiliana na kuhabarishana.

“Hata salamu yake anayotumia mara nyingi ni ile inayotengeneza nembo ya Freemason ya “V” na bikari hasa kwenye kukunja kidole cha mwisho cha mkono,” kilisema chanzo kimojawapo kwenye Mtandao wa YouTube na kuongeza;

ALAMA ZA USHINDI

“Angalia cheni zake anazovaa zina alama za ushindi dhidi ya kifo. “Kwa kawaida cheni hizo pia huwa na maandishi yanayosomeka ‘In Hoc Signo Vinces’ kwa Kilatini na kwa Kingereza husomeka ‘By this sign thou shalt conquer’ yakimaanisha kwa alama hiyo kuwa watashinda.”

MONDI AFUNGUKA

Katika mahojiano na gazeti hili kwa nyakati tofauti, Mondi anayekimbiza na wimbo wake wa Kanyaga amekuwa akieleza namna ambavyo jambo hilo limekuwa likimtesa.

Mondi amekuwa akiweka wazi kwamba yeye siyo Freemason na kwamba watu wenye wivu ndiyo wamekuwa wakisambaza habari hizo. “Siyo kweli bwana, mimi nazisikia tu hizi habari kama wengine. Sijui chochote. “Mimi ni mtu wa sala na mafanikio yangu naamini Mungu ndiyo kila kitu,” alisema Mondi.

MENEJA AFUNGUKA

Mmoja wa mameneja wa Diamond aliyezungumza na Gazeti la Amani juu ya ishu hiyo, Said Fela alianika ukweli wa anachokijua juu ya jambo hilo. “Kwenye mafanikio ya wasanii wetu yanasemwa mengi, wengine wanasema tunaloga na wengine hayo mambo ya Freemason, lakini ukweli hakuna kitu kama hicho. “Siri ya mafanikio ni kujituma kwa wasanii na uongozi makini hayo mengine hayana ukweli wowote,” alisema Fela.

FREEMASONI NI NINI?

Freemason ni jamii ya siri inayohusishwa na dini ya kishetani na watu wengi mashuhuri na maarufu wanatajwa kuwa wanachama wakiwemo viongozi wa nchi mbalimbali. Kwa upande wa wasanii mastaa kama Jay Z, Rihanna, Beyonce, Kanye West na Celine Dion wa Marekani ambao mafanikio yao yamekuwa yakidaiwa kuletwa kwa msaada wa nguvu za Freemason

Comments are closed.