WAKAZI wa Kimara Matosa wanaopita katika barabara ya King’ongo kuelekea maeneo ya Goba jijini Dar es Salaam, wamelalamikia kero ya ubovu uliokithiri wa barabara hiyo, inayowasababishia adha kubwa, hasa kipindi cha mvua.
Wakizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la kujaza kifusi kwenye maeneo korofi kwa kushirikiana na diwani wa Kata ya Saranga, Haruna Yusuf wananchi wa eneo hilo, wamesema barabara hiyo imekuwa kero kubwa kwao kutokana na kuwa na mashimo makubwa, hali inayosababisha watumie muda mrefu kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Naye diwani wa kata hiyo, Haruna Yusuf Mdoe aliyekuwa akishirikianana wananchi wake kumwaga kifusi kwenye maeneo yenye mashimo makubwa, amewaomba wadau mbalimbali kusaidia kurekebisha barabara hiyo ili kutatua kero hiyo inayowatesa wananchi wake.
NA DENIS MTIMA/GPL
Comments are closed.