The House of Favourite Newspapers

GLOBAL TV ONLINE -LIVE: Wakonta, Dickson Kukutana

Vijana wawili wa Kitanzania waliopooza, Wakonta Kapunda na Dickson, kesho wanatarajia kukutana nyumbani kwa Wakonta, Mbezi Juu jijini Dar kuelezea changamoto wanazokutana nazo katika hali waliyo nayo ya kupooza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo akimpa pole Dickso alipomtembelea katika Hospitali ya Ocean Road, Dar.

Wakonta ambaye ana uwezo wa kuandika stori na miswada ya filamu kwa kutumia ulimi, alipooza kiwiliwili chote wakati wa mahafali yake ya kidato cha sita, baada ya kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na mwanafunzi mwenzake.

Wakonta akiandika kwa kutumia ulimi.

Kwa upande wake, Dickson ambaye kwa sasa amelazwa Hospitali ya Ocean Road, Dar huku akiandika kitabu cha kuwapa wanadamu tumaini la kumtia mtu moyo, alipooza kuanzia kiunoni hadi miguuni wakati akiwa mwaka wa nne katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, baada ya kugundulika kuwa na saratani ya damu na TB ya uti wa mgongo.

Wankota akiwa amepumzika.

Tukio hilo la kihistoria litarushwa mubashara (live) leo Jumanne majira ya saa 10:00 jioni kupitia YouTube Chaneli ya Global TV Online hivyo usikose kufuatilia.

Kuyaona mazungumzo hayo SUBSCRIBE===>www.youtube.com/channel/UCCzlwMi5I8ievuVCikUoQIA

Comments are closed.