The House of Favourite Newspapers

Lipumba Atinga Mahakamani, Atoa Neno Sakata la Madawa

Lipumba akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama

Akitoka mahakamani

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayepingwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho, amefika mahakamani kusikiliza mwenendo wa mgogoro baina yake na maalim Seif Sharif Hamad ambapo baada ya kumalizika kwa kipindi cha mahakama, alipata fursa ya kuzungumza na waandishi wa habari.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama Kuu ya Tanzania, Lipumba alisema anaunga mkono suala la watuhumiwa wa madawa ya kulevya, kukamatwa na kuongeza kuwa serikali inapaswa kuungwa mkono katika suala hilo.

Lakini Lipumba aliongeza kuwa, serikali isikurupuke kuwapeleka watu mahakamani bila kuwa na ushahidi wa kutosha kwani suala hilo litaigharimu fedha nyingi katika kuendesha kesi hizo.

Kabla ya kuyazungumza hayo, Lipumba na wenzake walikuwa ndani ya mahakama ambapo kesi iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamni ya CUF dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Lipumba na wenzake ilikuwa ikisikilizwa.

Katika kesi hiyo, Jaji Kihiyo aliiahirisha hadi Machi 22, 2017 itakapotajwa tena.

Comments are closed.