The House of Favourite Newspapers

Wakurugenzi Wanne wa Halmashauri “Watumbuliwa Majipu”

0
1 (1)Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,George Simbachawane.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawane amewasimamisha kazi wakurugenzi wa nne  kwa  tuhuma  za  kuwahonga wakaguzi wa fedha  kutoka katika ofisi ya Mkaguzi mkuu wa  Hesabu za  serikali (CAG) ili wapewe hati  safi huku Halmashauri hizi zikiwa na ufisadi .
Wakurugenzi  waliosimamishwa  kazi  ni   Elizabeth Chitundu wa Halmashauri za Misenyi mkaoni Kagera, Ally Kisengi wa Halmashauri ya Nanyumbu mkaoni Mtwara  na  Abdalla Mfaume wa Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita.
Pia,Waziri Simbachawene   amemsimamisha kazi  mkurugenzi Halmashauri ya  Tunduma Mkoani  Mbeya Bi Halima Ajali  ili kupisha uchunguzi kutokana matumizi mabaya ya madaraka ikiwa ni pamoja na kuwatumia watoto wake katika shuguli za halmashauri na kuwalipa posho na kusababisha upotevu wa mapato.
Aidha, Waziri Simbachawane pia ameziagiza mamlaka husika kuwasimisha kazi watendaji wa ofisi ya mkaguzi wa Hesabu za Serikali nchini,CAG  waliohusika kupokea rushwa kutoka kwa wakurugenzi hao ili watoe  hati safi kwenye Halmashauri hizo huku zikiwa na ubadilifu wa fedha za Umma.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana Jijini Dar es Salaam,Waziri Simbachawene amesema Wakurugenzi hao wamegundulika  baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na wizara yake
Akibainisha makosa ya kila mkurugenzi,Waziri Simbachawene amesema Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misenyi, Bi Chitundu  alimwagiza  mweka hazina wake Majaliwa Bikwato atoe rushwa ya Milioni tatu kwa maafisa wa  ofisi ya CAG kwa lengo la kuficha kasoro walizoziabini katika ukaguzi huo  huku akijua ni kosa kisheria. Watumishi wa  wa ofisi ya CAG  waliopokea pesa hizo ni Stevin Buawa,John Elias pamoja na Kilembi Mkole
Katika Halmashauri ya Nanyumbu, Simbachawene amesema  kuwa  tarehe 26 Juni 2015, mkurugenzi wake bwana Kasengi pamoja na mweka hazina Pasco Malowo na mwasibu Emmanuel Mugesa walimkabidhi fedha Milioni 3 na laki tano  afisa wa ofisi ya  CAG  kwa lengo la kutoa hati safi
Waziri Simbachawene amesema mwezi Novemba mwaka jana , Mkurugenzi wa Halmashauri  ya  Mbogwe mkoani Geita Abdalla Mfaume na mweka hazina wake waliwapatia milioni 16  maafisa wakaguzi wa ofisi ya CAG  ili wafiche ufisadi walioubaini
Amesema katika Halmashauri hiyo pia kumegundulika kuwepo na ufisadi mkubwa ikiwemo malipo ya mishahara hewa pamoja na malipo ya milioni 200 yaliotolewa pasipo kuwa na Stakabadhi
Leave A Reply