The House of Favourite Newspapers

WAKUZA MISULI KWA KUJIDUNGA MADAWA HATARI

 

Tony ‘Hulk’ Geraldo (49) na Alvaro ‘Conan’ Pereira (50) wakionyesha misuli yao ya mikono iliyopanuka kwa kutumia madawa ya Potenay B12.
Misuli ya Geraldo yenye mzingo wa sentimita 71.12 na Conani sentimita 63.5 ilivyo baada ya kutumia madawa kwa zaidi ya miaka 30.
Pereira alipokuwa hajaanza kutumia madawa hayo.
Geraldo alivyokuwa kabla.
Ndugu hao wakiwa katika mazoezi yao ya kila siku.

 

NDUGU wawili wa kiume, Tony ‘Hulk’ Geraldo  (49)  na Alvaro ‘Conan’ Pereira (50)  wa Brazil wamekuwa wakijidunga madawa hatari ya Potenay B12  ili kunepesha misuli ya mikono tangu walipokuwa hawajafikia umri wa miaka 20.

 

Matokeo yake,  jamaa hao wanaoishi jijini Rio de Janeiro,  hivi sasa Hulk ana misuli yenye ukubwa wa mzunguko wa inchi 28 ambazo ni sawa na sentimita 71.12 na Conan inchi 25 ambazo ni sentimita 63.5.

 

Pamoja na kutumia madawa hayo, ndugu hao hufanya mazoezi kila siku na kutumia ratiba maalum ya chakula.  Geraldo anasema hula kila baada ya masaa matatu, hususani mayai, viazi mviringo na nyama.  Pereira hula mara nne kwa siku, wote wakitaka kuingiza nguvu ya kipimo cha kalori cha 4,000 hadi 6,000.

 

Madawa wanayoyatumia hutumiwa kwa ajili ya wanyama kama vile farasi.  Mke wa Pereira, ambaye mara ya kwanza walikutana kwenye ‘gym’ na watoto wake saba, wanamuunga mkono katika kupanua umbo lake.  Kwa upande wa Geraldo ambaye ana watoto watatu na aliyeoa miaka 27 iliyopita, mke wake hapendi atumie madawa hayo.

 

“Mke wangu hapendi kabisa.  Mimi nafurahia hali hii, kama hapendi itabidi kila mtu afuate njia yake,” anasema Geraldo anayeongeza kwamba huwa anamwambia mkewe kwamba ni yeye tu asiyempenda, kwani wanawake wengine wanalipenda umbo lake.

 

Kwa kawaida huwa wanakula ndizi 12 na mayai 12 kabla ya kuanza mazoezi, ambapo kupanuka kwa miili yao kuna wakati kumewafanya wakashindwa kupita katika milango kadhaa.

 

Pereira aliyeanza kutumia madawa hayo akiwa na umri wa miaka 15 anasema alishawishika kufanya hivyo baada kuona misuli ya kaka yake inatanuka.  Wote wawili wanasema walianza kufanya hivyo baada ya kujiona walikuwa vimbaumbau (wembamba) mno.  Wakati huo Geraldo alikuwa na uzito wa kilo 49 na Pereira 70.

 

Wawili hao pia wanakiri kwamba mtu aliyewapa nia ya kupanua miili yao ni mcheza sinema maarufu, Arnold Schwarzenegger,  hasa alipoigiza katika filamu ya Conan The Barbarian.

 

Pamoja na yote hayo, hivi sasa wanadhibiti utumiaji wa madawa hayo, mbali na kwamba madaktari wamewaonya wayaache sasa kwani ngozi za miili yao haziwezi kutanuka zaidi ya hapo.

 

 

WALUSANGA NDAKI/MITANDANO/MASHIRIKA YA HABARI

Comments are closed.