The House of Favourite Newspapers

Walimu, Wazazi Wakutana Kupongezana Mafanikio Ya Sekondari Ya Wasichana Ya John The Baptist

0
Baadhi ya wazazi wakiwa kwenye mkutano huo.

Dar es Salaam 11 Februari 2023: Wazazi na walezi waaswa kuwekeza kwenye elimu ili kuvuna matunda mazuri kwenye elimu kwa watoto wao.

Akizungumza katika mkutano wa wazazi, walezi  na walimu wa Sekondari ya Wasichana ya The John Baptist iliyopo Boko Basihaya jijini Dar, Mkurugenzi wa shule hiyo, Daisy Mayanja amesema kuwa kwa sasa wanajiandaa kupokea wanafunzi wa kidato cha tano hivyo basi amewaasa wazazi na walezi kuwahi kufanya maandalizi mapema ya kuwapeleka shuleni hapo ili watoto waweze kupata elimu iliyo bora na matokeo mazuri.

“Shule yetu imejipanga na kujiwekea mikakati mathubuti ili kuvuna matunda mazuri mwakani kwa watahiniwa wetu ikiwemo kufanya special programs za masomo kwa wanafunzi wa vidato vya mitihani wakati wa likizo ndefu na fupi ikiwa ni wanafunzi wa kidato cha sita.

Makamu  Mkuu wa shule hiyo, Samson Sixbert, akizungumza wakati wa mkutano huo.

“Wakiwa wanatarajia kufanya mtihani wao mwanzoni mwa mwezi wa tatu ili waendelee kunolewa kwa ajili ya mtihani huo, wanafunzi wa kidato cha pili na cha nne watabaki likizo ndefu ya mwezi wa sita na fupi ya mwezi wa tisa.

“Kumaliza muhutasali ndani ya nusu muhula wa kwanza mwezi wa tatu  kwa kidato cha nne ili waweze kufanya vizuri mitihani ya mock ambayo inatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi wa tano.

“Inatakiwa tuwe tumeshamaliza muhutasali na kufanya marudio, kutoa ushauri nasaha kwa kuhamasisha watoto wa kike kupenda masomo ya sayansi na hasa hesabu ili kuondoa dhana iliyojengeka vichwani kuwa hesabu ni ngumu na haiwezekani”. Alisema Mkurugenzi huyo.

Baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri mtihani wa kidato Cha nne 2022 walioalikwa shuleni hapo.

Baada ya kusema hayo mkurugenzi huyo amehitimisha kwa kuwahimiza wazazi na walezi kuwanunulia wanafunzi vitabu vya kiada na ziada na kuwaomba wazazi na walezi wasiwacheleweshe kwa maksudi wanafunzi hao kurudi shuleni pindi shule zifunguliwapo kwa sababu mpaka leo hii kuna wanafunzi bado hawajarudi shuleni na wala hawajahama.

Amesema baadhi yao huwa wanapotea na kurudi kipindi cha mitihani kitu ambacho hupelekea wanafunzi kutofanya vizuri kwani huenda kufanya mtihani pasipo kuwa na maandalizi ya kutosha.

Kuhusu suala la kutolipa ada mkurugenzi huyo amesema kutolipa ada kwa wakati si kitu kizuri kwani hupelekea mwanafunzi kurudishwa nyumbani mara kwa mara kitu ambacho hupelekea wanafunzi kukosa masomo na kusababisha kutokufanya vizuri mitihani yao.

“Upungufu wa vitabu vya ziada na kiada kwa wanafunzi hufanya mazoezi yaliyopo kwenye vitabu baadhi ya wazazi waliahidi ofisi ya taaluma kuwa wataleta vitabu lakini mpaka sasa hivi ni wazazi wachache walioweza kuleta vitabu au kulipia.

“Baadhi ya wazazi wa wanafunzi wa vidato vya mitihani kupinga umuhimu wa special programs, hivyo kitotimiza makubaliano ya malipo ya programs ambayo hutumika kuwalipa walimu wa part time, (CANOSA na FEZA) na malipo ya overtime pindi walimu wakimaliza kufanyakazi muda wa ziada,” amesema.

Aidha amewaomba wazazi na walezi kuhakikisha wanakuwa na vitabu pendekezwa angalau kimoja kwa kila somo ili kurahisisha zoezi la ufundishaji na ujifunzaji, wazazi kuwarudisha wanafunzi tarehe husika ya kufungua shule ili walimu waanze kuwaandaa wanafunzi wote kwa pamoja ndani ya muda uliokusudiwa.

Pia ameeleza kuwa wazazi kuhakikisha wanalipa ada kamili ya robo muhula ili kuepusha mwanafunzi kurudishwa nyumbani sababu ya ada, kwa wazazi wenye wanafunzi wa vidato vya mitihani kuhakikisha wanachangia gharama zilizotajwa kwa ajili ya programs za likizo.

Mkurugenzi huyo pia ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani zake za dhati kwa wazazi wote walishiriki mkutano huyo na kuwaomba kutimiza yale yote yaliyozungumzwa ili mwaka ujao waweze kuwa na ufaulu mzuri zaidi.

Alimalizia kwa kueleza kuwa katika kutoa motisha kwa wanafunzi, shule imetoa udhamini wa ada (shilingi milioni moja) kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha nne 2022 na kuendelea na masomo ya kidato cha tano shuleni hapo Julai mwaka huu.

Leave A Reply