The House of Favourite Newspapers

Waliokamatwa Sakata la ‘Unga’ Wafikishwa Mahakamani Kisutu, Wema Hajatokea

TID kushoto akiwa na watuhumiwa wengine
Watuhumiwa wakichuchumaa.     

WASANII na wafanyabiashara waliokuwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili taratibu za kisheria ziweze kufuata kama ilivyoagizwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Kamishna Simon Sirro.

Miongoni mwa wasanii na watu maarufu waliofikishwa mahakamani hapo mpaka sasa ni Khalid Mohamed ‘T.I.D’, Video Queen Tunda Sebastian, Petit Man, Babuu wa Kitaa, Dogo Hamidu, Rommy Jones, Rachel pamoja na na Lulu Diva.

Aidha, kulingana na taarifa za mwanahabari wetu aliyepo eneo la tukio muda huu, Wema Sepetu bado hajaonekana mahakamani hapo.

Tutaendelea kukujuza kinachojiri.

PICHA NA MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS

Sakata la Unga; Watuhumiwa Wapewa Dhamana na Masharti Matatu Mahakamani

Comments are closed.