The House of Favourite Newspapers

WALIOKATAA FEDHA ZA UWOYA GLOBAL WAPEWA KITITA

Mhariri Mshauri wa Magazeti ya Global, Elvan Stambuli (kulia) akimkabidhi kitita cha fedha mwanahabari wa Global TV, Hilaly Daudi,  baada ya kuonyesha weledi wa kutogombea fedha wakati mwigizaji wa Bongo Movies, Irene Uwoya,  alipowamwagia fedha waandishi wa habari waliojitokeza katika Ukumbi wa Hyatt Kilimanjaro jijini Dar, hivi karibuni kwenye mkutano ulioitishwa na wasanii wa tasnia ya filamu nchini.

UONGOZI wa Global Publishers umewapongeza kwa kuwapa kitita cha fedha wanahabari wake, Imelda Mtema na Hillary Daudi,  kwa kuonesha weledi wa kutogombea fedha wakati mwigizaji wa Bongo Movies, Irene Uwoya alipowamwagia fedha waandishi wa habari waliojitokeza katika Ukumbi wa Hyatt Kilimanjaro jijini Dar, hivi karibuni kwenye mkutano ulioitishwa na wasanii wa tasnia ya filamu nchini.

Tukio hilo la Uwoya lilielezwa kuwa la kidhalilishaji kwa waandishi ambao walipigana vikumbo kugombea fedha za msanii huyo.

Mmoja wa wahariri wa Magazeti ya Global Publushers, Sifael Paul (kulia),  akimkabidhi kitita cha fedha mwandishi wa magazeti hayo, Imelda Mtema.  baada ya kuonyesha weledi wa kutogombea fedha wakati mwigizaji wa Bongo Movies, Irene Uwoya alipowamwagia fedha waandishi wa habari waliojitokeza katika Ukumbi wa Hyatt Kilimanjaro jijini Dar, hivi karibuni kwenye mkutano ulioitishwa na wasanii wa tasnia ya filamu nchini.

AISEE Kama ULAYA! Tazama Safari ya Kwanza AIR TANZANIA Kuelekea MUMBAI

Comments are closed.