SULUHISHO LA UPUNGUVU WA NGUVU ZA KIUME

KwA muda mrefu sasa huwa tunaandika tatizo hili na kutoa ushauri. Kwa muda mrefu sasa suala hili la unyumba linajadiliwa sehemu mbalimbali. Jambo linalozungumziwa au kujadiliwa na wengi na kwa kipindi kirefu ujue kwamba ni jambo kubwa na suluhisho au ufumbuzi bado haujapatikana.

Tatizo hili ni kubwa kwa kuwa linagusa moja kwa moja maisha ya mtu kama ilivyo umaskini. Kila mwanaume anaweza kupata tatizo hili, haijalishi wewe ni nani, wadhifa wako, umri au upo wapi. Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume bado lipo na linaendelea kuwepo na ndiyo maana tafiti bado zinaendelea katika nchi mbalimbali za Ulaya na Amerika huku ipo haja ya kuanza utafiti hapa Tanzania.

UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Upungufu wa nguvu za kiume au kitaalam ‘ERECTILE DYSFUCTION’ na maana nyingine ‘IMPORTENCE’ au ukhanithi, ni mwanaume kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume na kuufanya uendelee kuwa na nguvu kwa kuendelea na tendo. ‘Inability to get and keep an erection firm enough for sex’. Tatizo hili linatokea mara mojamoja, siyo lazima kwamba una tatizo hili labda ni uchovu au msongo wa akili.

Endapo tatizo hili la upungufu wa nguvu za kiume linaendelea tu haliishi, basi linaweza kusababisha msongo wa mawazo na kukupotezea hali ya kujiamini na hata kuharibu uhusiano wako. Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume pia ni ishara ya uwepo wa magonjwa mengine mwilini.

AINA YA TATIZO LA UPUNGUVU WA NGUVU ZA KIUME

Tatizo hili limega wanyika katika maeneo matatu ambapo aina ya kwanza ni uume kushidwa kusimama au unasimama halafu unapoanza tendo unakosa nguvu na kulala. Aina ya pili ni kuwahi kumaliza tendo, mfano unapoanza tu tendo hilo

unamaliza kabla hata ya dakika tatu na aina ya tatu ya tatizo ni kutokuwa na hamu wala msisimko wa tendo hili, yaani upoupo tu, wengine hupata msisimko au hamu hadi wasikie wengine au waangalie picha za ngono. Tatizo hili uhusiana sana na wale wanaojichua au ‘MASTER-BATION’. Matatizo haya kwa mwanaume ni kama majanga kwani hujikuta unatumia muda mwingi na gharama kubwa kutibu

bila mafanikio.

DALILI ZA UGONJWA

Dalili za upungufu wa nguvu za kiume ni endelevu, zinapotokea huwa zinaendelea na hatimaye tatizo linakua kubwa zaidi ugonjwa huu huchukua muda mrefu hata miaka. Dalili hizi ni kushindwa kusimamisha uume unapohitaji kushiriki tendo, unashindwa kuendelea kusimamisha uume ‘trouble keeping an erection’ hupunguza au kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa kadiri siku zinavyoenda ‘reduce sexual desire’.

Hali hizi zina uhusiano mkubwa na kuwahi kumaliza tendo la ndoa ‘premature ejaculation’ au kuchelewa kumaliza ‘delayed ejaculatoin’. Hali hizi pia zina uhusiano mkubwa na uwepo wa magonjwa kama kisukari, magonjwa ya moyo au magonjwa yoyote sugu mwilini. Upungufu huu wa nguvu za kiume pia huambatana tena wakati mwingine na uchovu wa mwili, maumivu ya kichwa na mwili vya mara kwa mara.

CHANZO CHA TATIZO

Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na kutofurahia tendo ni tatizo la muda mrefu na sugu ambalo uhusisha ubongo, homoni na hali ya kisaikolojia ya mtu, mishipa ya fahamu, misuli ya mwili na mishipa ya damu kwa hiyo shida kubwa inaweza kuanza hapa. Msongo wa mawazo na matatizo ya akili yanaweza kusababisha tatizo hili likawa baya zaidi.

Wakati mwingine matatizo ya kimwili na kiakili huwa ni chanzo kikubwa katika tatizo hili la upungufu wa nguvu za kiume. Hofu katika uhusiano au hofu juu yako mwenyewe kwamba utadhurika au kuumia utakaposhiriki au huweza kukufanya uishiwe au upungukiwe na nguvu.

Itaendelea wiki ijayo.


Loading...

Toa comment