The House of Favourite Newspapers

Waliosambaza Video Za Prof Jay Mbaroni

0

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), linawashikilia Samuel Mhina, mwandishi wa mkurugenzi wa Mtandao wa Kijamii wa U-turn Connection, mkazi wa Temeke na wenzake 13 kwa tuhuma ambazo zinachunguzwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema watuhumiwa hao wanatuhimiwa kusambaza video za aliyekuwa Mbunge wa Mikumi na mwanamuziki maarufu, Joseph Haule ‘Prof Jay’ akiwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili bila kibali cha hospitali hiyo.

 

Kamanda Muliro ameongeza kuwa Jeshi la polisi pia liliwakuta na vifaa mbalimbali vya kielektroniki, ikiwemo kamera, kalamu za kiuchunguzi, miwani na kofia zenye camera, laptop na memory card ambavyo vyote vinachunguzwa na mamlaka husika ili kubaini uhusika wake na tukio la kusambazwa kwa video hiyo ambapo uchunguzi utakapokamilika, watafikishwa mahakamani.

Leave A Reply