The House of Favourite Newspapers

Wamiliki wa Malori Waendelea Kumlilia Rais Samia

0
Mwenyenyekiti wa Wamiliki wa Malori Wadogo na Wa kati (TAMSTOA) Chuki Shabani kulia akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kulia ni mjumbe wa kamati kuu ya TAMSTOA Mark Gama.

 

 

Wanachama wa Chama cha Wamiliki Malori Wadogo na Wa kati nchini, Tanzania Medium and Small Truck Owners Association (TAMSTOA) wameendelea kumuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan aendelee kuwasaidia kuwanasua wenzao wanaoendelea shikiliwa na malori yaliyobeba magogo nchini Zambia.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya TAMSTOA, Benjamini Mwapongo (kulia) akisistiza jambo wakati wakizungumza na wanahabari, kushoto ni mjumbe wa chama hicho, Mark Gama akimsikiliza kiumakini.

 

 

Wamiliki hao wamesema awali madereva zaidi ya 400 walikuwa wanashikiliwa nchini humo lakini kwa juhudi zilizofanywa na Rais Samia madereva wengi waliachiwa lakini kuna madereva kama 80 bado wanaendelea kushikiliwa nchini humo.

Mkutano huo uliofanyika Hoteli ya Double View Sinza, Dar ukiendelea.

 

 

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika Hoteli ya Double View iliyopo Sinza, Dar leo, Mwenyekiti wa TAMSTOA, Chuki Shabani akiwa na wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Mark Gama, Benjamini Mwapongo, Issa John na Salum Mkumbwa walianza na kumshukuru Rais Samia kwa juhudi zake za kufanikisha madereva hao kuachiwa na kurudi majumbani kwao.

Katibu Mkuu wa TAMSTOA, Issa John (kulia) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Salum Mkumbwa wakisikiliza kiumakini yaliyokuwa yakiendelea.

 

Chuki na wajumbe wa kamati kuu ya TAMSTOA wametoa shukrani nyingi sana kwa Mama Samia kwa kuwakomboa madereva hao waliokuwa wamezuiliwa nchini humo na kuishi katika mazingira magumu na kutenganishwa na familia zao kwa muda mrefu.

 

Pamoja na shukrani hizo wamiliki hao wameendelea kumuomba Mama Samia aendelee kuwapambania madereva hao zaidi ya 80 ambao wameendelea kuzuiliwa nchini humo.

HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL 

Leave A Reply