The House of Favourite Newspapers

Wanafunzi Royal College – Dar Waandamana

Wanafunzi hao wakiwa wamebeba mabango nje ya chuo hicho.

 

WANAFUNZI wa Chuo cha Uandishi wa Habari cha jijini Dar es Salaam, Royal College of Tanzania leo wameandamana wakipinga kuondolewa kwa baadhi ya walimu wao bila kupewa taarifa huku wakiulalamikia uongozi wa chuo hicho kwa kufanya maamuzi bila kuwashirikisha.

Wanafunzi wakiwa wamekusanyika.

 

Tukio hilo limetokea leo Februari 2, 2018 majira ya jioni ambapo wanafunzi hao walijikusanya nje ya majengo ya chuo hicho kilichopo Kinondoni huku wakijikusanya na kushikilia mabango yaliyoandikwa kupinga kilichotokea.

 

Aidha, wanafunzi hao wamefunga geti la lango kuu la chuo hicho huku wakizuia walimu wasitoke nje ya chuo hicho mpaka hapo watakapopata majawabu ya kuridhisha kuhusu madai ya wanafunzi hao.

Geti likiwa limefungwa.

“Uongozi wa chuo hauthamini Serikali ya wanafunzi chuoni, wamefanya mabadiliko ya walimu bila kutushirikisha, ghafla walimu hatuwaoni chuoni wala madarasani.

 

Wanafunzi wakiwa na mabango yao.

 

“Kuna mabadiliko ya kiutendaji ambayo wanatakiwa kuyafanya lakini hawafanyi. Mbaya zaidi kuna walimu wengine watatu wanatakiwa kuondoka na hatujapewa taarifaaa. hapa mambo ni moto,” alisema mmoja wa wanafunzi hao.

Hali halisi ilivyokuwa.

 

 

 

PICHA NA GLOBAL: WHATSAPP 0753 715 779

Comments are closed.