Wanajeshi wa China, Wamtembelea Mkuu wa Mkoa Dar (VIDEO)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza na wanahabari.

Mkuu wa Kikosi cha Maji wa China (Navy), Shen Hao, akielezea ujio wao hapa nchini.

Baadhi ya viongozi wa China wakiwa katika hafla hiyo.

Wakiwa katika picha ya pamoja.

VIONGOZI  wa jeshi la China leo wamemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ambapo amewaomba kumsaidia kuwapatia vifaa vya kutumiwa  na askari wa doria katika Bahari ya Hindi   ili waweze kukabiliana na wahalifu wenye kuuza na kusafirisha madawa ya kulevya.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar, Makonda ameeleza kuwa ujio wa viongozi  hao umejadili pia masuala mengi ya ushirikiano baina ya watu wa nchi hizi mbili na kuhakikisha usalama wa wao na ushirikiano mwingine wa nyanja mbalimbali.

Naye Mkuu wa Kikosi cha Maji  cha China (Navy),  Shen Hao, amepongeza juhudi za mkuu huyo wa mkoa  hasa za kuhakikisha anapambana na watu wanaoingiza madawa ya kulevya wakipitishia pembezoni mwa Bahari ya Hindi na akasema ushirikiano wa nchi yake  na nchi ya Tanzania utaendelea kuwa imara.

Stori:  DENIS MTIMA/GPL 

 

VIDEO: Wanajeshi wa China, Wamtembelea Mkuu wa Mkoa Dar 

Loading...

Toa comment