The House of Favourite Newspapers

Wanakijiji Wamkataa Mwenyekiti Aliyepita Bila Kupingwa

0

IKIWA ni wiki moja limepita tangu kufanyika uchaguzi wa serikali za mitaa nchini, ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipata ushindi wa kishindo baada ya kushinda kwa asilimia 99.9, mambo mapya yameanza kuibuka kuhusu uchaguzi huo.

 

Huko mkoani Mwanza, wananchi wa Kijiji cha Ng’ombe, wilayani Misungwi wamemkataa mwenyekiti aliyepita bila kupingwa wa CCM, Zakayo Magondo, kwa maelezo kuwa kiongozi huyo hawafai, huku wakimtuhumu kwa vitendo vya rushwa na uchonganishi.

 

Akizungumza, mmoja wa wakazi wa kijiji hicho amesema awali katika kura za maoni ndani ya chama, mgombea huyo aliyepita bila kupingwa siye aliyeshinda kwenye kura za maoni, kwani yeye alipata kura 100 na kitu, huku mwenzake akipata kura 300, lakini cha ajabu akaletwa huyo aliyeshindwa.

 

Wananchi hao wamesema kuwa Zakayo amekuwa mwenyekiti kwa miaka 15 na hakuna chochote alichofanya ndani ya kijiji hicho, hivyo hawamtaki tena.

 

Wakiendelea kutoa maoni yao kuhusu kiongozi huyo, wananchi wamesema huwa hawasomewi taarifa za mapato na matumizi ya kijiji, huku suala la ulinzi na usalama ndani ya kijiji hicho nalo likizidi kuzorota kwa sababu watu wanang’ang’ania madarakani bila kuchaguliwa na wananchi.

 

Akizungumza katika kikao hicho, Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga aliwataka wananchi hao kuwa na utulivu huku akieleza kuwa kwa vile kiongozi huyo alipitishwa kwa kufuata taratibu, hivyo hata kuondolewa kwake kunapaswa kufuata taratibu.

 

Amesema lazima kwanza kiti hicho kibaki wazi, ili mkurugenzi wa uchaguzi aweze kuitisha tena uchaguzi.

Leave A Reply