The House of Favourite Newspapers

Wananchi wafurahia ofa  ya Danube

Mmoja wa wateja waliotembelea katika  duka la Danube  la GSM Group, lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam,  Miss Tanzania 2005, Nancy Sumari (katikati) akionyeshwa na Afisa Mauzo wa Duka hilo, Habiba Said baadhi ya biddhaa zinazouzwa dukani hapo kwa BEI CHEE.
Afisa Mauzo wa Duka la Danube la GSM Group, Habiba Said (kushoto) akimuonyesha moja ya  chombo cha kuwekea matunda, Miss Tanzania 2005, Nancy Sumari (kulia) ambaye alitembelea duka hilo.

Siku chache baada ya GSM Tanzania kuzindua kampeni ya “BEI CHEE” yenye lengo la punguzo la bei kwa asilimia 70% ili kuwanufaisha wateja wake hususani msimu huu wa maandalizi ya sikukuu kwa kununua bidhaa mbalimbali katika maduka yao ya DANUBE yaliyopo katika Mall ya Mlimani City na Pugu,Wananchi wengi ambao tayari wameanza kunufaika na kampeni hiyo jijini Dar es Salaam wamesema kampeni hiyo ni silaha ya kuondoa umaskini kwenye familia nyingi na  ikitumiwa ipasavyo itapendezesha nyumba zao na  wengi kuwanunulia zawadi wanaoishi  nje ya Dar es Salaam.

 

Wakiongea kwa nyakati tofauti baada ya kutembelea duka la Danube lililopo jijini Dares Salaam mlimani city, baadhi ya wateja wamesema kuwa endapo wananchi wengi wenye vipato vya chini au vya juu wataichangamkia kampeni hii wengi wao ndoto zao za kumiliki bidhaa nzuri zenye kupendezesha majumbani kwao au maofisini zitatimia.

 

“Mmoja wa wateja akiongea na waandishi wa habari katika duka hilo lililopo mlimani city jijini Dar es Salaam kuhusiana na Kampeni hiyo Nancy Sumari ambaye alikuwa Miss Tanzania 2005 ambaye kwa sasa anajishughulisha na shughuli zake za ujasiriamali alisema kama ambavyo tumeelekezwa ni kampeni ya kipee kabisa ambayo haijawahi kutolewa hapa nchini kwa ajili ya kutunufaisha sisi tukiwa kama wateja wa maduka haya”,Alisema.

 

Aliongeza kuwa kwa jinsi alivyopata tu habari kupitia njia ya mtandao alifunga safari yake kuja kununua bidhaa mbalimbali kwani hakutegemea kabisa katika maisha yake kama angekuja kusikia Danube ina kampeni ya aina hii kwani bidhaa zao zinauzwa kwa bei chee kabisa na ndiyo maana ameacha kazi zake zote za ujasiliamali na kuja kununua bidhaa hizo na amegundua kuwa Danube ni mkombozi kwa wajasiriamali nchini na ametoa wito kwa watanzania  kuichangamkia frusa hiyo, Alisema Sumari.

 

Akiongelea kampeni hii inayoendelea,Meneja Uendeshaji wa maduka ya Danube Tanzania yaliyopo chini ya GSM Group,Haji Mfikirwa amesema kuwa kampeni ya“BEI CHEE”imelenga kuwanufaisha  wateja wa GSM na wananchi kwa ujumla nchi nzima na kwa jinsi gani wanaweza kunufaika na msimu huu wa maandalizi ya sikukuu ili wapate kufurahia na familia zao kwani wamesikia  kilio chao na kuamua kuwaletea bei chee.

 

“Tunafurahi kuona wateja wetu wameipokea kampeni hii vizuri kwa kuona hivi tunafarijika sana na tunapenda kutoa wito kwa wale wote ambao awajapata nafasi ya kutembelea maduka yetu watembelee ili waje kunufaike na bidhaa zetu nyingi zenye bei chee kabisa, kwani kampeni kama hizi zinafanyika mara chache sana kwa mwaka na hii ndiyo frusa ya kipekee”. Alisema Mfikirwa.

Comments are closed.