The House of Favourite Newspapers

Wanaopinga Taliban: Tupo Tayari kwa Mazungumzo

0

 

KIONGOZI wa Kundi la Wapiganaji wanaopinga kundi la Taliban nchini Afghanistan anayeongza vita vikali dhidi ya Taliban katika Bonde la Panjshir amesema yuko tayari kuingia katika mazungumzo ya amani.

 

Ahmad Massoud alisema anaunga mkono mpango, uliowasilishwa na maulama wa kidini, kwa suluhu iliyojadiliwa, na akatoa wito kwa Taliban kusitisha mashambulizi yao.

 

Hapo awali, ripoti zilidokeza kwamba Taliban ilikuwa imepiga hatua kubwa kulitwaa eneo la Panjshir.Jimbo hilo, kaskazini mwa mji mkuu Kabul, ni mfano maarufu zaidi wa pingamizi dhidi ya utawala wa Taliban.

 

Kikundi hicho cha Kiisilamu kilidhibiti Afghanistan yote wiki tatu zilizopita, kikichukua mamlaka huko Kabul mnamo Agosti 15 kufuatia kuanguka kwa serikali inayoungwa mkono na nchi za Magharibi.

 

Katika chapisho kwenye Facebook, Massoud alisema National Resistance Front of Afghanistan (NRF), ambayo inajumuisha wanachama wa zamani wa vikosi vya usalama vya Afghanistan na wanamgambo wa ndani, watakuwa tayari kuacha mapigano ikiwa Taliban itaacha mashambulio yao. Hakukuwa na jibu la haraka kutoka kwa Taliban.

 

Leave A Reply