The House of Favourite Newspapers

Wanasayansi Wagundua Uhai Sayari ya Venus

0

WAZO kwamba viumbe wanaoishi wanaelea katika mawingu ya sayari ya Venus ni uwezekano uliopo. Lakini hilo ni kwa mujibu wa wataalamu wa angani baada ya kugundua kitu kilichopo angani ambacho hakiwezi kuelezeka.

 

Ni gesi kwa jina Phosphane PH3, molekyuli ilioundwa kutokana na atomu moja ya Phosphorous na tatu za Hydrogen. Phosphine, ni kitu chenye sumu na chenye harufu mbaya walichokigundua katika mawingu hayo ya sayari ya Venus na ambacho kinaonekana kuwa ishara ya uhai katika sayari hiyo.

 

Duniani, Phosphine inahusishwa na uhai. Inapatikana katika viumbe vidogo vinavyoishi katika koo za wanyama kama vile Pingu ama maeneo yenye mazingira duni ya hewa kama vile vidimbwi vya maji ardhini. Ni gesi inayoweza kuzalishwa katika viwanda.

Kwanini gesi hii ipo  kilomita zipatazo 50 kutoka ardhini?

Profesa Jane Greaves wa chuo kikuu cha Cardiff na wenzake wanauliza swali kama hilo. Na wamechapisha taarifa katika jarida la asili ya anga zinazoelezea ugunduzi wao kuhusu Phosphine katika sayari ye Venus, pamoja na uchunguzi waliofanya ili kujaribu kuonesha kwamba molekyuli hii inaweza kuwa na chanzo asilia na kisicho cha kibaiolojia. Lakini kwa sasa wamechanganyikiwa.

Juu ya kila kitu kinachojulikana kuhusu sayari, hakuna aliyefanikiwa kuelezea chanzo cha Phosphine kibaiolojia. Na sio hata kwa kiwango kilichogunduliwa. Hii ina maana kwamba ni vyema kugundua kwamba kuna ishara za uhai katika sayari hiyo.

”Tangu nianze kazi yangu nimekuwa na hamu kujua iwapo kuna uhai katika maeneo mengine ya ulimwengu, hivyo basi nafurahi kwamba hilo linawezekana,”  alisema Profesa Greaves.

Lakini ni kweli tunawashinikiza watu wengine kutuambia kile ambacho huenda tumekikosa. Stakabadhi zetu pamoja na data ziko wazi – hivyo ndivyo jinsi sayansi inavyofanya kazi.

 

Je ni lipi la kuvutia?
Sayari ya Venus haipo katika orodha ya uwezekano wa uhai katika maeneo mengine ya mfumo wa sayari. Ikilinganishwa na dunia, ni jahanam. Asilimia 96 ya anga yake ina gesi ya kaboni. Kiwango cha joto katika sakafu yake ni zaidi ya nyuzi 400.

Vifaa vya angani vilivyotua katika sayari hiyo vimechukua dakika chache kabla ya kuharibika. Hata hivyo, umbali wa kilomita 50 kaskazini viwango vya joto sio vya juu. Hii ndiyo sababu inaaminika kwamba iwapo kuna uhai katika sayari ya Venus basi ni katika eneo hili.

Je ni kwa nini tunapaswa kuwa na hofu?
Mawingu yake ni mazito na yanamiliki kati ya asilimia 75 hadi 95 za tindikali ya Sulphuric, ambayo ni hatari kwa viumbe vinavyoishi duniani.

Je ugunduzi huo umepokelewaje?

Kundi hilo lina wasiwasi, likisisitiza kuwa halijadai kwamba limepata uhai katika sayari ya Venus, lakini lina sema kwamba wazo hilo linahitaji kuchunguzwa zaidi kwa kuwa wanasayansi pia wanasaka njia za kibaiolojia ama hata za kikemikali ili kulielezea.


Je hilo litatatuliwa vipi?
Kwa kutuma kifaa kwenda kufanya uchunguzi hususan anga ya sayari ya Venus. NASA hivi majuzi iliwauliza wanasayansi, kufanyia kazi ujumbe utakaokwenda mwaka 2030. Roboti za kutumia anga zimependekezwa kusafiri kupitia mawingu ya Venus. Urusi ilifanya hivyo  mwaka 1985.

Leave A Reply