The House of Favourite Newspapers

Wanaume Wazidi Kumtesa Zari

0

 

ANATESEKA! Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na yanayoendelea kwa mjasiriamali maarufu nchini Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’ kwani kila kukicha wanaume wameonekana kumtesa.

 

Wanamtesa kivipi? Ni hivi; Zari amekuwa akionekana kwenye picha na wanaume mbalimbali ambapo mara nyingi huwa anawakata sehemu ya shingoni na kuacha kiwiliwili tu ili watu wasimuone sura huyo mhusika.

Kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram, gumzo kubwa ni kuhusiana na picha ya Zari iliyovuja hivi karibuni akiwa amevaa sare na mwanaume mmoja huku akiwa amemkumbatia kwa kumshika kimahaba kiunoni jambo ambalo lilisababisha gumzo na watu kudai anateseka.

 

Baada ya picha hiyo kusambaa, watu walidai kuwa mwanaume huyo inawezekana ndiyo yule King Bae ambaye Zari alisema hawezi kumweka wazi kwa kuwa hayo ni mambo yake binafsi.

“Huyu Zari anateseka sana maana anapiga picha na huyu mara huyu ili tu kutuumiza roho sisi timu flani, kwa mapicha haya atakuwa anafanya hivyo ili kumrusha roho mzazi mwenzake, Nasibu Abdul ‘Diamond’,” aliandika mdau mmoja kwenye mtandao wa Instagram.

 

Zari na Diamond walimwagana Februari mwaka jana wakiwa wamejaaliwa watoto wawili lakini tangu hapo mwanamama huyo amekuwa akiweka picha mbalimbali za mwanaume ambapo huficha sura. Jambo ambalo wadadisi wa mambo wanaeleza kuwa ni njia mojawapo ya kuwarusha roho watu pamoja na familia ya Diamond.

STORI: GLADNESS MALLYA, RISASI

Leave A Reply