The House of Favourite Newspapers

Waoga maji ya sumu, wababuka

0

SAMSUNG CAMERA PICTURES

Mmoja wa waathilika wa maji hayo akiwa amebabuka shingono.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti hivi karibuni, baadhi ya wakazi wa vijiji hivyo wamesema licha ya maradhi hayo waliyopata yanayotokana na kemikali zinazosababishwa na machimbo hayo, bado hawapati msaada wowote kutoka kwa wamiliki wa kampuni hiyo.

Mwikwabe Mwita Waigama (70), mkazi wa Nyangoto ambaye ugonjwa umesababisha ahamie kwa kijana wake Makamba Mwikwabe anayeishi Kijiji cha Matongo, anasema anaendelea kuteseka bila kupona tangu alipooga maji ya sumu katika kisima cha asili cha Nyabirama.

SAMSUNG CAMERA PICTURES

Mfereji unaopitisha maji hayo ya sumu ukielekea karibu na makazi ya watu.

‘’Mimi nilioga maji ya sumu ya mgodi katika kisima chetu cha asili na nikaanza kujikuna, pamoja na kushughulikiwa na familia yangu, Hospitali za Shirati, Tarime, Nyamongo na nyinginezo bado nimepooza mwili, angalia nilivyo,’’ alisema mzee Mwikwabe Mwita Waigama ambaye mwili wake umebabuka.

Naye Chacha Kiguha Babere ambaye alikataa kuhama kwa sababu ya fidia ndogo ya shilingi 1,700,000 mwaka 2010, anaendelea kuishi kwa mateso katika makazi yake kitongoji cha Ntarechagini Kijiji cha Komarera.

Alisema yeye na familia yake wanaishi na magonjwa ya ngozi, yaliyotokana na uchafuzi wa mazingira uliofanywa na shughuli za uchimbaji, achilia mbali adha zingine zikiwemo kubomoka kwa ukuta wa nyumba yake kutokana na mitetemo na kelele zinazosababishwa na ulipuaji wa baruti.

SAMSUNG CAMERA PICTURES

Bwawa linalohifadhi maji hayo ya sumu.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Komarera, Nyamaganya Manga, alibainisha wazi kuwa licha ya mgodi huo kushindwa kuwafidia malipo ya kuhamishwa watu wote waliomo ndani ya mita 200, pia umeharibu miundombinu ya mto Tighite na kufanya maji yake kukosa mwelekeo na yaliyosababisha hasara ya mashamba ya wakazi 20 wa kijiji chake.

Kwa mujibu wa Bodi ya Maji ya Ziwa la Bonde La Victoria (LVBWB) katika uchunguzi wake wa Septemba 2014, maji yanayotiririka katika makazi ya watu kutoka bwawa la Nyabirama yana sumu, hivyo kuweka wazi kuwa ni hatari kwa afya za watu na mifugo.

SAMSUNG CAMERA PICTURES

Ng’ombe akiwa amekufa baada ya kunywa maji hayo ya sumu.

Hiyo ilikuja baada ya n’gombe zaidi ya 168 kufa kwa  nyakati tofauti tangu mwaka 2012 hadi sasa. Katika kikao cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma, Waziri Sospeter Muhongo aliahidi kufika Nyamongo na kutembelea wakazi wa vijiji vinavyozungukwa na mgodi huo huku Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina akitoa siku 14 kwa suala hilo kupatiwa ufumbuzi.

 

Leave A Reply