The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Wapigadebe Watimuliwa Vituo vya Daladala Dar

0
Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetoa siku tatu kwa wapigadebe wote kwenye vituo vya daladala jijini Dar kuhakikisha wameondoka kwenye vituo hivyo, kwani katika uchunguzi wao wamebaini kuwa wengi wao si wapigadebe bali ni wahalifu wanaojihusisha na uporaji.

 

Akitoa tamko hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar, Lucas Mkondya amesema kuwa kuanzia Jumatatu, Agosti 14 mwaka huu, mpigadebe yeyote asionekane kwenye kituo chochote cha daladala, huku akisema kuwa atakayekutwa kituoni kuanzia siku hiyo atakiona.

 

“Kuanzia Jumatatu, asionekane mpigadebe yetote kwenye vituo vya daladala, tumebaini wanajihusisha na uporaji, wanapanda kwenye daladala wanakwenda na abiria hadi anaposhuka na wao wanashuka, akitembea akafika kwenye kichochoro wanamkaba wanamuibia, hiyo hatutaki, waondoke wote wakafanye kazi nyingine,” alisema Kamanda Mkondya.

 

Aidha Kamanda huyo ameeleza kuw, makondakta hawatakiwi kuwaruhusu wapigadebe kufanya kazi hiyo kwenye magari yao, kondakta wa daladala atakayepatikana amemruhusu mpigadebe wote watakamatwa.

VIDEO: MSIKIE KAMANDA AKIZUNGUMZA

Leave A Reply