The House of Favourite Newspapers

WCB Wagomea Tuzo za Basata… Listi Ipo Hapa

0

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limetangaza majina ya wasanii mbalimbali wanaowania tuzo za muziki zikiwa na vipengele 51 ambapo miongoni mwa waliotajwa, hakuna msanii hata mmoja kutoka lebo ya WCB inayoongozwa na Diamond Platnumz.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Matiko Mniko, wasanii 1360 walipeleka kazi zao ambapo baada ya mchujo wa kamati maalum yenye wajumbe 100, ndipo orodha hiyo ilipotangazwa.

“ulitaka utoaji wa tuzo huu uwe huru, wasanii wenyewe wajipendekeze na wapi wanaona wanawanapaswa kuwa na baada ya mchujo, wateule waliopatikana ndio hao,” amesema Mniko.

Siku chache zilizopita, Diamond alisikika katika mahojiano na chombo kimoja cha habari, akisema wasanii wote waliopo chini ya WCB hawatashiriki kwenye tuzo zozote za ndani.

Leave A Reply