The House of Favourite Newspapers

Wasafi Washangaza Mashabiki Wamepata Wachumba lakini Ajabu Hakukuwa na Ndoa

0

WASANII wengi wa lebo ya Wasafi Classic Baby ( WCB) walibahatika kuwa na wachumba lakini ajabu ni kwamba hakukuwa na ndoa yoyote iliyofungwa au kudumu. Tuwaangazie warembo wanne ambao walipata wachumba Wasafi lakini waliachana bila ndoa, au ndoa kuvurugika na uhusiano wao umevunjika.

FAHYMA Ni mwanamitindo chipukizi ambaye alijizolea umaarufu baada ya kuzaa na staa wa muziki wa Bongo Fleva kutoka kwenye lebo ya WCB, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, penzi lao liling’aa na kuwa gumzo mitandaoni baada ya kuonekana wakiambatana kila mahali na kutajwa kwamba ni wachumba hivyo kuwafanya watu kuzidi kuwafuatilia kwa karibu.

Mapichapicha ya pamoja yalikuwa kama yote, huku kila mmoja akimposti mwenzake kwa mbwembwe na kuandika maneno matamu yaliyoashiria penzi zito mioyoni mwao na uchumba ulioshamiri.

Kuna kipindi Fahyma alivunja ukimya na kusema kwamba ndoa itafungwa Desemba 12, mwaka 2019 lakini kwa bahati mbaya mwaka ukapita bila ya ndoa na ghafla habari zikasambaa kuwa wawili hao wameshabwagana na baada ya kufuatilia sana ikaonekana kwamba mrembo Nanah aliyeshiriki kwenye video ya wimbo wa ‘I Love You’ wa Rayvanny ndiye kasababisha wanandoa hao kumwagana baada yakudaiwa kutoka kimapenzi na msanii huyo.

Fahyma alikubali kwamba hawana ndoa tena na Rayvanny.

TANASHA Huyu ni mtangazaji wa kituo cha redio NGR nchini Kenya, ambaye umaarufu wake ulianza kujulikana zaidi baada ya kutoka kimapenzi na bosi wa WCB, Nasibu Abdul ‘Diamond’ au ‘Mondi’.

 

 

Urembo wake ukazidi kumvutia Mondi hadi kujikuta akishindwa kuzuia hisia zake na kumuweka hadharani kama mchumba tofauti na alivyofanya kwa baby mama wake mwingine Hamisa Mobetto.

Haikuchukua muda sana mwanamama huyo akabeba ujauzito na akafanikiwa kujifungua mtoto wa kiume aliyeitwa Naseb Junir, hatujakaa sawa mara penzi lao likaanza kuingiwa na mdudu baada ya kudaiwa kumwagana huku miongoni mwa sababu zilizofanya penzi lao kuvunjika ni pamoja na video queen anayefahamika kwa jina la Malaika, ambaye ameshiriki katika video ya ‘Jeje’ ya msanii huyo, kudaiwa kuwa wapenzi.

Picha za Diamond na video queen huyo zilianza kusambaa kwenye magazeti pendwa na mitandaoni huku kila mmoja akiongea lake, wapo waliosema Diamond ameshalala na mrembo huyo, hivyo Tanasha hana chake na wengine wakasema sio kweli bali ile ni kazi tu kama zilivyo kazi nyingine.

Mpaka hivi sasa wawili hao tayari wameshaachana na mwanamama huyo amerejea nchini kwao Kenya.

SARAH Alikuwa ni mke halali wa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ ambaye alikuwa WCB.

Mapenzi yao yalionekana kushamiri na kupendwa na watu kwa kuwaaminisha watu kwamba hawawezi kuachana, kwani Sarah aliweza kuonekana kwenye wimbo wa Harmo wa ‘Niteke’ na kuweza kusilimu ili kufunga ndoa ya Kiislam.

Licha ya penzi lao kushamiri, lakini likaja kuingia shubiri ghafla. Mara baada ya Harmo kutoa wimbo wake wa ‘Bed Room’, huku mwanadada mwenye umbo tata Nicole Joyberry akiwa kama video queen ndipo kisa kilipoanzia, baadhi ya watu walisema kuwa Harmo hawezi kumuacha hivihivi mrembo huyo bila ya kutoka naye.

Mara video ya Sarah kumfanyia vurugu msichana huyo ikaanza kuzagaa kwa kasi mitandaoni, baadaye wakaachana na sasa ndoa hakuna.

ZARI Huyu naye ni raia wa Uganda waliwahi kuishi na bosi wa WCB Mondi kama wachumba lakini ikaishia Zari kuzalishwa watoto wawili na Mondi na na uchumbaukaisha.

Makala; Elvan Stambuli, Ijumaa

WASTARA JUMA AIBUA MAZITO KIFO cha SAJUKI – “USIOLEWE, WANAUME WATAKUTESA”…

Leave A Reply