The House of Favourite Newspapers

Wasanii Waliotwaa Tuzo Za Filamu 2023, Wafundishwa Jinsi Ya Kulinda ‘Brand’ Zao, JB, JOTI Watajwa

0
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Dr. Kiagho Kilonzo akiwapa somo wananii hao.

Dar es Salaam, 30 Desemba 2023: Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo Kitengo cha Bodi ya Filamu, imeendesha mafunzo kwa wasanii waliotwaa tuzo za filamu mwaka huu zilizofanyika Ukumbi wa The Super Dome Masaki jijini Dar hivi karibuni.

Akifungua mafunzo hayo, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Dr. Kiagho Kilonzo amewataka wasanii hao kuzingatia mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kujitambua na kuishi kadiri ya hadhi waliyonayo na kulinda brand zao ili wasiweze kuchuja kama baadhi ya waliowahi kuwa mastaa wa muda mfupi na kupotea.

Msanii JB na wenzake wakiwa kwenye mafunzo hayo ambapo msanii huyo alifika kwenye mafunzo hayo kama mtoa mafunzo.

Dr. Kilonzo aliwashauri wasanii hao kuiga mfumo wa maisha ya watu kama wasanii wenzao Jb na Joti ambao kwa miaka mingi wako kwenye tasnia ya uingizaji na bado hawajachuja.

Aliwatolea mifano ya mastaa mbalimbali akiwemo aliyekuwa mwanamasumbwi mashuhuri ulimwenguni Mike Tyson ambaye kwasasa hakuna anayefuatilia anachofanya baada ya kupoteza umaarufu.

Akiwapa mafunzo wasanii hao, Dr. Kilonzo aliwaambia wasanii hao kuwa kulinda hadhi kunaanzia hata unapotakiwa kujitambulisha sehemu mfano ulishawahi kuwa mshiriki wa tuzo fulani na hukupata ni vyema ukajitaja ushiriki wako kwenye tuzo hizo kwani hata kushirikishwa pia ni heshima tosha ingawa wengi wanasahau hilo.

Kwa upande wake Joti aliyefika kwenye mafunzo hayo kama msanii asiyechuja aliyapongeza mafunzo hayo na kusema serikali imefikiria kitu cha muhimu sana kuja na mafunzo hayo.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwa makini kusikiliza.

Amesema unapofanikiwa kulinda ‘bland’ yako ndivyo unavyoweza kufanya taasisi mbalimbali ziendelee kukutumia katika matangazo yao nawe kuzidi kujiingizia kipato siku zote za maisha yako kwa maana brand yako ikichuja hakuna wa kuendelea kukutumia.

“Tatizo kubwa sisi wasanii na mastaa wengine unaweza kupata ustaa kwa tukio moja lakini shida inakuja katika kuulinda huo ustaa hiyo ndiyo changamoto na hapa leo ndiyo tunafundishwa kuulinda ustaa wako”. Alisema Joti.

Joti akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na mafunzo hayo.

Naye msanii Jb alisema mafunzo hayo yatasaidia kutengeneza mastaa wa kudumu na hivyo kuwasaidia kupata wasanii wa kuwatumia maana kwa muda mrefu wamekuwa wakiwatumia akina Wema, Uwoya, Wolper kwakuwa kwa muda mrefu tangu wapate ustaa hao hakuna wasanii wapya wanaojitengenezea brand na kubaki na haohao kila siku.

Naamini baada ya mafunzo haya tunaweza kupata mastaa wapya na kuturahisishia kutafuta washiriki wa filamu zetu.  HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS/ GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply