The House of Favourite Newspapers

Washia Waadhimisha Kifo cha Mtume Muhammad kwa Maandamano ya Amani Dar

washia-3
washia-4 washia-5 washia-6  washia-2 washia-1

WAUMINI wa Dhehebu la Shia nchini, leo wamefanya maandamano ya amani kwa ajili ya kuadhimisha kifo cha Mtume Muhammad (S.A.W.W) wakiwa na ujumbe wa “Mtume Muhammad (S.A.W.W) ni rehema kwa watu wote.”

Maadhimisho hayo yamefanyika kuanzia maeneo ya Ilala – Boma hadi Viwanja vya Pipo, Kigogo-Post  jijini Dar es Salaam yakiratibiwa na Sheikh Hemed Jalala wa Chuo cha Imamu Swadiq kwa kushirikiana na Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheria ya Tanzania (T.I.C).

Mtume Muhammad (S.A.W.W) alifariki dunia tarehe 28 (Safari, mwaka wa 11 Hijria) katika mji mtakatifu wa Madina.

“Ndugu zangu Waislamu tuna kila sababu ya kuadhimisha siku ya kifo cha Mtume kama ambavyo tumekuwa tukiadhimisha kuzaliwa kwake, kama ambavyo tumekuwa tukiadhimisha kidunia siku ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu J.K Nyerere,” alisema Sheikh Jalala.

 

halotel-strip-1-1

 

Comments are closed.