The House of Favourite Newspapers

WASHINDI TUSUA MAISHA NA GLOBAL KUKABIDHIWA ZAWADI ZAO LEO

Washindi wa Tusua Maisha na Global walipokabidhiwa zawadi zao wiki jana.

WAKATI washindi wa droo ya saba na nane wa Shindano la Tusua Maisha na Global wakitarajiwa kukabidhiwa zawadi zao leo, Ijumaa Agosti 24, 2018, Simba Ramadhan, mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam ameibuka mshindi wa kwanza katika droo ya tisa na kujishindia pikipiki mpya.

Mshindi akikabidhiwa pikipiki.

 

Wengine waliong’ara katika droo ya tisa ni Anna Mbise, mfanyabiashara kutoka Arusha aliyejishindia dinner set na Hussein Mtipa wa Ifakara, Morogoro aliyejishindia jezi.

Washindi walipokabishiwa zawadi zao.

 

Wanaotarajiwa kukabidhiwa zawadi zao leo Ijumaa ni Said Katambo wa Nachingwea, Lindi na Jackson Bwire wa Ukerewe, Mwanza waliojishindia pikipiki, Nobert Benjamin wa Nyamagana Mwanza na Boniface Malick wa Bunju A jijini Dar es Salaam waliojishindia dinner set.

Mshindi akiwa kwenye pikipiki aliyokabishiwa.

 

Wengine ni Benard Kasembe wa Pugu Mwakanga aliyejishindia head phones za kisasa za Beats by Dre, Gasper Ndimbo, mkazi wa Miseko, Mkuranga na Ally Bakari, Mkazi wa Vikindu waliojishindia jezi.

Mshindi kutoka Mbeya akikabishiwa zaawadi ya diner set.

 

“Tutawakabidhi zawadi zao leo, kwa wale wa mikoani tumeshawasiliana nao na kuwapa utaratibu wa namna ya kutuma wawakilishi watakaokuja kuwapokelea zawadi zao na ambao hawana wawakilishi hapa Dar es Salaam, watatumiwa zawadi zao hukohuko waliko.

Mshindi kutoka Kibiti akikabidhiwa zawadi ya ada ya shule ya mwanaye.

 

“Lengo letu ni kurudisha shukrani kwa wasomaji wetu, kwa kutufanya kuwa kampuni ya kwanza kuchapisha magazeti mengi zaidi yanayofika karibu kila sehemu ndani ya nchi yetu,” alisema Abdallah Mrisho, Meneja wa Kampuni ya Global Publishers.

Ili kuwa miongoni mwa washindi, nunua gazeti lolote linalochapishwa na Global Publishers kati ya Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra kisha funua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya namna ya kushiriki.

Itume namba maalumu inayoonekana juu ya kuponi kwa njia ya meseji kwenda namba 0719386533. Hakikisha unahifadhi kuponi au gazeti lako kwani linahitajika wakati wa kuchukulia zawadi vigezo na masharti vinazigatiwa.

Comments are closed.