The House of Favourite Newspapers

Wasichana 2 Wakutwa Wakipigana Busu Juu ya Paa, Wafikishwa Mahakamani

_92680984_moroccocourt

MARRAKESH, MOROCCO: Wasichana wawili waliokutwa wakipigana busu katika paa la nyumba wamefikishwa mahakamani katika Mji wa Marrakesh nchini Morocco wakishtakiwa kwa madai ya kujihusisha na tabia za wapenzi wa jinsia moja, mmoja wa mawakili wao waliambia chombo cha habari cha AFP.

Wasichana hao ambao mmoja ana umri wa miaka 16 na mwingine miaka 17, walishtakiwa kwa kushiriki tendo lililo kinyume na maumbile yao. Wawili hao walikamatwa mwezi uliopita baada ya kuripotiwa na familia zao.

Walipatikana wakikumbatiana na kupigana busu juu ya paa, hivyo kulingana na kosa hilo wanakabiliwa na vifungo vya miezi sita hadi miaka mitatau jela.

Licha ya kusomewa hayo, wasichana hao walikana mashtaka hayo ambayo yalisomwa kama ripoti ya polisi kwamba walikuwa wakifanya vitendo vya wapenzi wa jinsia moja na kusema kuwa uhusiano wao ni wa kirafiki.

Chanzo: BBC

halotel-strip-1-1

Binti Panya Road Asimulia Mazito

Comments are closed.