The House of Favourite Newspapers

Cuba Kuomboleza Kifo cha Fidel Castro kwa Siku 9

Fidel Castro

Nchi ya Cuba itaomboleza kwa siku tisa kifo cha Fidel Castro, anayejulikana kwa siasa zake za kimapinduzi, aliyetawala taifa hilo kwa miongo kadhaa.

Mwili wa Fidel aliyefariki dunia juzi Ijumaa akiwa na umri wa miaka 90, utachomwa moto hadi kuwa majivu kama alivyotaka yeye, ambapo majivu yake yatazungushwa katika msafara maalumu kote nchini humo kabla ya kuzikwa katika makaburi ya Mji wa Santiago, Desemba 8, mwaka huu.

Akiwa kiongozi mwenye mrengo wa kushoto na mwanamapinduzi msifiwa, alipendwa na kuchukiwa na watu mbalimbali kote duniani.

Watu wengi katika Mji Mkuu wa Havana walidondokwa na machozi kwa kifo cha kiongozi huyo shujaa aliyeweza kukabiliana na Marekani katika uwanja wa kidiplomasia kwa miongo kadhaa, licha ya mbinu nyingi zilizofanywa za kutaka kumuua.

Hata hivyo Waasi wa Serikali ya Castro walisherehekea kifo chake kote duniani walikotorokea.

halotel-strip-1-1

MAKONDA NA KAMANDA SIRRO MGUU KWA MGUU TANDALE KUTAFUTA MAKAHABA

Comments are closed.