The House of Favourite Newspapers

Wasira Amshangaa Lissu Kwenda Chato “Hakuna Aliyemtukana Kama Yeye” – Video

0
Stephen Wasira

MWANASIASA mkongwe nchini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira ameeleza kushangazwa na hatua ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu kutangaza kwenda Chato mkoani Geita kumshtaki Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na mpango wa uwekezaji wa bandari ya Dar es Salaam unaoendelea.

Wasira amesema hakuna mtu aliyewahi kumtukana Rais John Magufuli akiwa madarakani kama kiongozi huyo.

“Jana (Chadema) walikuwa Kagera, yule muongo mwandamizi akasema ataenda Chato kwa Magufuli kushtaki mambo ya bandari… hakuna mtu aliyemtukana Magufuli wakati wa urais wake kama yeye. Amesahau ya jana. Anaenda kufanya nini Chato? naomba wamsubiri wampe haki yake kwa kumzomea,” amesema.

Pamoja na hayo Wasira amesema siri ya kelele za viongozi na makada wa CCM wanaozunguka nchi nzima kuelimisha umma kuhusu uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam, ni upotoshaji unaofanywa na watu wanaoumezea mate urais.

Amesema watu hao ambao hakuwataja, walidhani Rais Samia Suluhu Hasssan atakapoingia madarakani atashindwa kutekeleza majukumu yake ndani ya siku 100.

Akizungumza leo tarehe 29 Julai 2023 katika viwanja vya Kawe jijini Dar es Salaam Wasira amesema baada ya Rais Samia kutekeleza majukumu yake kikamilifu, sasa watu hao wamenuna.

“Wakisema tukamseme,watamsemea wapi na kuhusu nini kwa sababu maji yapo, madarasa, huduma za kijamii zipo. Unamsema wapi? Hivyo ili kumchafua lazima kuzulia jambo la uongo kuwa ameuza bandari… ameuza nchini,” amesema.

Amesema nchi ipo mikononi mwa CCM na chama hicho hakiwezi kuuza nchi.

“Tunalinda Uhuru hatuwezi kuuza bandari. Wakisema uongo kesho tunafika kuujibu. Wakae chonjo hatuwezi kuruhusu uongo uwape mamlaka katika nchi yetu,” amesema.

Leave A Reply