The House of Favourite Newspapers

Wasomaji Arusha Waapa, Lazima Msimu Huu Mshindi wa Nyumba Atoke Kaskazini

shinda-nyumba-arusha-1

KIPYENGA PRIIIII!, Hatimaye lile shindano kubwa nchini la bahati nasibu ya Shinda Nyumba Msimu wa Pili linaoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers, ambao ni wachapshaji wa magazeti ya Amani, Championi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi na Uwazi limezinduliwa rasmi kwa wakazi wa Jiji la Arusha na vitongoji vyake juzi Jumatano.

shinda-nyumba-arusha-2Msomajiwa magazeti yanayochapishwa na Global Publishers akichana kuponi ya Shinda Nyumba kwenye gazeti baada ya kujaza.

Katika uzinduzi huo wasomaji wa magazeti ya Global Publishers walionekana fursa ya uzinduzi huo kwa kujitokeza kwa wingi na kujaza kuponi maradufu huku wakiapa kuwa awamu hii lazima mshindi atokee Kanda ya Kaskazini.

shinda-nyumba-arusha-3Wasomaji wakichangamkia magazeti ya Global Publishers ili wajaribu bahati yao.

Miongoni mwa wasomaji wa magazeti pendwa ya Globa Publishers, Ndugu Joshua Laiser aliapa kwa kusema,

shinda-nyumba-arusha-4“Msimu huu ni zamu yangu ya kujishindia nyumba kwani huu ndio mwaka wangu wa kumiliki mjengo Dar es Salaam baada ya Nelly Mwagosi (mshindi wa nyumba msimu ulityopita), nitahakikisha nanunua kila gazeti la Global Publishers linapotoka, najaza kuponi, nakata kuituma kama maelekezo yanavyonitaka.” Alisema Laiser.

shinda-nyumba-arusha-5Wasomaji wakiendelea kujaza kuponi.

Katika uzinduzi huo, Shinda Nyumba ilitembelea Ofisi za Global Publishers Arusha, Stendi Ndogo ya Mabasi ya Mikoani, Kilombero, Ngarenaro, Soko Kuu, Mianzini, Sakina, Majengo, Kwa Mrombo, Kwa Iddi, Arusha Mjini hadi Kijenge.

shinda-nyumba-arusha-6Mwakilishi wa Global Publishers, ndugu Chocks Francisco Chokala aliwashukuru watu wote waliojitokeza kwa wingi na kuwaomba waendelee kununua kila siku magazeti ya Global Publishers na akawaombea dua kwa Mungu ili bahati ziwaangukie wana Kanda ya Kaskazini.

shinda-nyumba-arusha-7Kushiriki SHINDA NYUMBA, nunua gazeti lolote linalochapishwa na Kampuni ya Global Publishers ambayo ni Amani, Championi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi na Uwazi kasha jaza kuponi iliyoko ukurasa wa pili, kata kuponi hiyo na uipeleke kwa wakala aliye karibu nawe au ofisini kwetu, Mwenge-Bamaga jijini Dar es Salaam.

Comments are closed.