The House of Favourite Newspapers

Chale 21 Alizochanjwa Diamond…

dai1

Daimond Platnumz

DAR ES SALAAM: Ijumaa Januari 20, 2017 Alama 21 zinazodaiwa ni chale zinazopatikana mgongoni mwa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ zimezua mambo baada ya juzikati picha yake kutupiwa mtandaoni ikizionesha kwa uwazi na kuibua mjadala mzito.

Picha hiyo iliyotupiwa mtandaoni ilimuonesha Diamond akiwa kwenye moja ya shoo alizofanya hivi karibuni huku akizungushiwa eneo ambalo lilionekana kuwa na chale, jambo lililowafanya wadau kibao wazijadili.

Mmoja wa mashabiki hao aliandika hivi: “Duh! Huyu jamaa hakamatiki aisee, kwenye shoo zake ni nyomi, anang’ara kimataifa, utajiri wake usiseme, au ndiyo tuseme hizi chale zake alizochanjwa ndiyo sababu?

“Yaani kama ni hivyo na mimi aniambie tu kachanjwa wapi ili na mimi niende kwa huyo mganga wake.” dai-3

Daimond Platnumz

Mwingine akaandika hivi: “Acheni zenu, huyu Mond ana nyota yake tu, hizo chale inawezekana ilikuwa ni tiba ya kawaida.

Akizungumza na Ijumaa, mmoja wa wasanii anayefanya poa licha ya nyota yake kutong’ara sana, D-Malick alisema:

“Unajua nasikia tu kwamba huwa wasanii wakubwa wanaendaga kwa wataalam ‘kutengenezwa’ ili washaini, niliona picha moja inaonesha Diamond akiwa amechanjwa chale mgongoni, aisee kama ndizo zinamfanya awe na mafanikio hayo makubwa ipo siku nitamfuata anielekeze na mimi niende.”

Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Diamond kuzungumzia mjadala huu ulioibuka kuhusiana na chale zake zikihusishwa na kung’ara kwake lakini hakuweza kupatikana mara moja.dai-2

Daimond Platnumz

Hata hivyo, siku za nyuma Diamond aliwahi kuongea na gazeti hili na kusema kwamba, madai kuwa kufanya kwake vizuri kwenye muziki kunatokana na mambo ya kishirikina siyo kweli bali juhudi binafsi ndizo zilizomfikisha mahali alipo.

“Mafanikio yangu hayatokani na mambo ya kishirikina, juhudi na maarifa ndiyo siri ya mafanikio yangu,” aliwahi kusema hivyo Diamond.

 

Comments are closed.