The House of Favourite Newspapers

Wasomaji: Betika linatuingizia fedha ndefu katika kubeti

WASOMAJI wa Gazeti la Betika kutoka maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam, wamefunguka kuwa gazeti hilo kila siku zinavyozidi kwenda mbele linawafanya kupata fedha nyingi  kwani hulitumia katika kubeti na wanashinda.

Gazeti la Betika ambalo ni mahususi kwa masuala ya kubeti, tangu liingie mtaani wadau wengi wa masuala ya kubeti wamekuwa wakilisifia.

Leo Jumatano, maofisa masoko wa Kampuni ya Global Publishers ambayo ndiyo inachapisha gazeti hilo, iliingia mtaani maeneo ya Mbagala na kuzungumza na wasomaji mbalimbali.

 

“Gazeti hili uzuri wake ni kwamba linakurahisishia katika kazi hizi za kubeti, kwa watu kama sisi ambao tunajishughulisha na kubeti, linatusaidia sana.

“Kila siku linapokuwa mtaani lazima nilichukue kwa sababu linatolewa bure, basi huwa silikosi, ndani yake kuna maujanja ambayo yananisaidia katika kushinda,” alisema mmoja wa wasomaji hao.

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, alisema kuwa mapokeo ya gazeti hilo kila siku yanazidi kuwa juu hali inayodhihirisha kwamba wasomaji hasa wazee wa kubeti walikuwa na kiu kubwa ya bidhaa kama hiyo.

“Gazeti hili ni mahususi kwa ajili ya ishu nzima ya kubeti, lina makala nyingi zinazoelezea kampuni mbalimbali za kubeti, lakini pia humo ndani kuna odds zinazomfanya msomaji kupata njia rahisi za kubeti.

“Kikubwa ni kwamba, wasomaji wetu wamekuwa wakitupa mrejesho mzuri ambao unatupa mwanga kwamba gazeti hili lilikuwa linahitajika kwa muda mrefu,” alisema Mgema.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 ambazo zote ni za rangi, mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya na hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18.

Comments are closed.