The House of Favourite Newspapers

Wasomaji: Betika linatusaidia sana

WAKATI Gazeti la Betika likiwa limefikisha wiki 16 mtaani, wasomaji mbalimbali wamezidi kulipongeza kwa jinsi lilivyokuja tofauti.

 

 

Gazeti hilo ambalo huchapishwa na kusambazwa na Kampuni ya Global Publishers, hutolewa bure kwa wenye umri kuanzia miaka 18.

Betika ambalo lina kurasa 20 ambazo zote ni za rangi, lina makala na odds za kampuni mbalimbali za kubeti.

 

 

Leo Jumatano ambapo gazeti hilo huingia mtaani, Timu ya Maofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers ilitembelea mitaa ya Magereza, Vingunguti na Banana jijini Dar es Salaam na kuzungumza na wasomaji kadhaa.

“Kiukweli gazeti hili lipo tofauti sana, linaturahisishia katika masuala mazima ya kubeti kutokana na namna lilivyo.

 

 

“Ukilisoma ndani kuna odds na makala za kimataifa ambazo zinachambua timu, kwa ufupi ukilisoma kwa umakini Betika, linakupa mwanga mzuri wa kubeti na kushinda,” alisema msomaji mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Amos Charles.

Naye Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, aliendelea kukazia kwamba ndani ya Betika kuna nafasi kwa watangazaji kuleta matangazo yao ili kujitangaza.

 

 

“Wasomaji wetu tunawajali sana, kila siku tumekuwa tukiweka vitu vizuri ndani ya gazeti letu hili ambalo huwa tunalitoa bure.

 

 

“Bado tunapokea matangazo, hivyo hii ni fursa ya watu ambao wanataka kutangaza nasi kuleta matangazo yao kwetu,” alisema Mgema.

Comments are closed.