The House of Favourite Newspapers

Wasomaji Betika Popobawa, Magomeni Makanya, Mapipa Walivyolichangamkia

MAPEMA leo Jumatano,Novemba 20,2019 timu ya maofisa masoko ya Global Publishershers imetembelea maeneo ya Popobawa, Magomeni Makanya, Magomeni Mapipa na maeneo mengine ya  Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuendelea kulitangaza zaidi Gazeti la Betika ambapo baadhi ya wasomaji wameonekana kulichangamkia vilivyo wakati timu hiyo ikiligawa bure. Betika  hutolewa bure kwa wenye umri kuanzia miaka 18, linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers na huingia mtaani kila Jumatano.
Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, lina takwimu za ligi tofauti na matangazo mbalimbali ya biashara. Baadhi ya wasomaji waliokutana na timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, walizidi kulisifia gazeti hilo kuwa gumzo kila kona ya nchi na kurahisisha kwenye masuala ya michezo ya kubeti.
Gazeti hilo heshima yake imeendelea kukua siku hadi siku na sasa lina watangazaji wengi ambao wanatangaza biashara zao kupitia Betika kwa bei nafuu. Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Global Publishers katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.
Matukio katika Picha:

Comments are closed.