The House of Favourite Newspapers

Wasomaji wa Amani, Majohe Wachangamkia Safari ya Dubai

0

1 George Msyaliha msomaji wa Amani, mkazi wa Kitunda (katikati) akilisoma gazeti hilo. Anayemshuhudia ni Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda.

WASOMAJI wa Gazeti la Amani katika mitaa ya Majohe, Kitunda, Kivule na maeneo mengine ya jiji la Dar es Saalaam, leo Alhamisi Agosti 18, wamejitokeza kwa wingi kulichangamkia gazeti hilo ambapo wameonesha kuvutiwa na Chemsha Bongo ya kwenda Dubai.

2.Ofisa Masoko wa gLobal, Yohana Mkanda (kulia akiwaonesha wasoamji wa Amani ukurasa wenye Chemsha Bongo.Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda (kulia) akiwaonesha wasomaji wa Amani ukurasa wenye Chemsha Bongo.

Timu ya gazeti hilo ilitinga kama kawaida maeneo hayo kwa lengo la kuonesha wasomaji mabadiliko makubwa yaliyofanywa ndani ya gazeti hilo ikiwa ni sambamba na kuwepo kwa safu mpya kama vile Kijiwe cha MC Pilipili, Nafasi za Kazi, Sindano za Mastaa, Mtu Kati na nyingine nyingi.

3.Msomaji wa Amani aitwaye Nyamboge Chacha (kulia) mkazi wa Kivule Dar akielekezwa jambo na Mkanda.Msomaji wa Amani, Nyamboge Chacha (kulia) mkazi wa Kivule Dar akielekezwa jambo na Mkanda.

Wasomaji wengi walilinunua gazeti hilo na wengine kusogea karibu na gari la matangazo lililokuwa likipita maeneo hayo na kueleza kuwa wanalikubali kwa kila kitu.

4.Wasoamaji wa Amani wakimzunguka Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda (mwenye fulana nyeupe kulia) kujua namna ya kushiriki Chemsha Bongo hiyo).Wasomaji wa Amani wakimzunguka Yohana Mkanda (mwenye fulana nyeupe kulia) kujua namna ya kushiriki Chemsha Bongo hiyo).

Akizungumza mmoja wa wasomaji hao, Mohamed Ngongo alisema kinachomvutia zaidi ni namna linavyochimbua habari za mastaa na kuandika na pia matukio ya kijamii ndiyo sababu kubwa inayomfanya kulipenda gazeti hilo.

5.Gaspar Mwanjali (kushoto) akilisoma gazeti la Amani.Kulia ni ofis Masoko wa Global Yohana Mkanda akimfafanulia jambo.Gaspar Mwanjali (kushoto) akilisoma Gazeti la Amani. Kulia ni Yohana Mkanda akimfafanulia jambo.

“Jamani nalipenda sana Gazeti la Amani kwani ndilo  gazeti bora hapa Bongo kwa sasa lenye habari zake za kuvutia za wasanii mbalimbali, habari zake, hadithi na makala zinanifanya nisiache kulinunua,” alisema Mohamed Ngongo mkazi wa Kivule.

6.Wadau wa Gazeti la Amani wakipozi na gazeti hilo eneo la Kitunda Relini.Wadau wa Gazeti la Amani wakipozi na gazeti hilo eneo la Kitunda Relini.

Aidha msomaji wa gazeti hilo unaweza kushiriki katika chemsha Bongo iliopo ukurasa wa pili katika gazeti hilo na kujishindia kuanzia Sh. 500,000 hadi tiketi ya kwenda Dubai na kuponda raha katika hoteli ya kifahari kwa muda wa siku tatu.

7.Mkanda akimfafanulia jambo msaoamaji wa Amani jinsi ya kushiriki Chemsha Bongo inayopatikana ndani ya gazeti hilo.Mkanda akimfafanulia jambo msomaji wa Amani, Proscovia Lasway jinsi ya kushiriki Chemsha Bongo inayopatikana ndani ya gazeti hilo.

Naye Mhariri wa gazeti hilo, ameendelea kutoa wito kwa wasomaji wa Magazeti ya Global Publishers ya Ijumaa Wikienda, Risasi, Amani na Championi, isipokuwa Ijumaa linalouzwa Sh.1000,  kuendelea kulinunua Amani kwa bei ya Sh.500 kwani thamani ya kilichomo ndani yake ni zaidi ya bei hiyo.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply