The House of Favourite Newspapers

WASOMAJI WALISHUKURU GAZETI LA BETIKA

BAADHI ya wasomaji wa gazeti namba moja na la kijanja linalohusu ishu nzima za kubeti lijulikanalo kwa jina la BETIKA, wamelishukuru kutokana na kurahisisha mambo yao ya kubeti.

Gazeti hilo ambalo hutolewa bure kila Jumatano, hii ni wiki ya tatu lipo mtaani na tangu litue mtaani, limekuwa likipewa sifa kemkem.

Leo Jumatano, timu nzima ya Maofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers ambayo ndiyo inachapisha gazeti hilo, ilitinga mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ikiwemo Kinondoni, Magomeni, Jangwani na Tandale kwa ajili ya kulinadi gazeti hilo.

 

 

Mmoja wa wasomaji wa gazeti hilo, alisema: “Kiukweli gazeti hili limekuwa mkombozi mkubwa kwetu hasa sisi tunaojihusisha na masuala ya kubeti kwa sababu inaifanya kazi yetu kuwa rahisi, humu tunapata maujanja yote ya kubeti, kabla ya kubeti huwa tunajua nini cha kufanya ili iwe rahisi kushinda.”

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, alisema kuwa mapokea ya gazeti hilo kila siku yanazidi kuwa juu hali inayodhihirisha kwamba wasomaji hasa wazee wa kubeti walikuwa na kiu kubwa ya bidhaa kama hiyo.

“Gazeti hili ni mahususi kwa ajili ya ishu nzima ya kubeti, lina makala nyingi zinazoelezea kampuni mbalimbali za kubeti, lakini pia humo ndani kuna odds zinazomfanya msomaji kupata njia rahisi za kubeti.

 

“Tangu liingie mtaani, tumepata mrejesho mzuri kwamba wasomaji wanalihitaji sana, hivyo tutaendelea kuwapa vitu vizuri wasomaji wetu ili kukata kiu yao,” alisema Mgema.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 ambazo zote ni za rangi, mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya.

 

MWANDISHI WETU

Comments are closed.