The House of Favourite Newspapers

Wasoshalisti washinda uchaguzi Hispania

 

Waziri mkuu wa Hispania, Pedro Sanchez anayeongoza chama cha Kisoshalisti, ameshinda katika uchaguzi uliofanyika jana Jumapili kwa kupata idadi kubwa ya viti bungeni.

 

Licha ya kupata idadi ya viti ambavyo vinamwezesha kuunda Serikali peke yake, Sanchez atalazimika kushirikiana na vyama vingine vilivyopata idadi kubwa ya viti ili kuwa na umiliki kamili kwenye bunge.

 

Chama cha  Sanchez kimepata asilimia 29 ya kura, kikipata viti 123 katika bunge la nchi hiyo lenye viti 350.

Vyama vya mrengo wa kushoto ambavyo vilikuwa kimya tangu kuangushwa kwa utawala wa kifalme wa Francisco Franco mwaka 1975, vimepata asilimia 10 ya viti bungeni  kwa mara ya kwanza.

 

Sanchez ametangaza kuanza mazungumzo hivi karibuni na vyama vya siasa, akiwaambia waungaji wake mkono kwamba mustakabali wa nchi hiyo umeshinda na mambo ya zamani yameshindwa.

Comments are closed.