WASTARA ATOBOA SIRI YA KUPENDA KUOLEWA

Wastara Juma

LICHA ya kuolewa zaidi ya mara tatu, msanii mwenye jina kubwa kwenye tasnia ya filamu Bongo, Wastara Juma amesema siri ya kufanya hivyo ni kutafuta faraja ya moyo wake na wanaye kupata baba sahihi ingawa wakati mwingine mambo yamekwenda asivyotarajia.  

Wastara aliiambia Star Showbiz ya Uwazi katika mnuso f’lan uliokuwa maeneo ya Posta jijini Dar.

“Unajua mimi ni binaadamu kama wengine ambapo nimekuwa nikitamani kuishi na mume ili nijisikie niko na mwenzangu na wanangu wawe na mtu wa kumuita baba ingawa wakati mwingine mambo yamekuwa yakienda tofauti,” alisema Wastara.

 

Alipouliza juu ya sababu za kuachika mara kadhaa katika ndoa zake, msanii huyo alikataa kuziweka wazi na kuishia kusema kila mmoja amekuwa na sababu zake. Kuhusu utayari wa kuolewa tena kwa siku za hivi karibuni msanii huyo amesema hawezi kusema kuwa yuko tayari au hayuko tayari kwa kuwa yeye ni binaadamu na mawazo yake yanabadilika kutokana na mazingira na wakati.

RICHARD BUKOS

Toa comment