The House of Favourite Newspapers

WASTARA HALI TETE TENA !

Wastara Juma.

LICHA ya Februari, mwaka huu kupatiwa matibabu nchini India, bado hali ya staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma ni tete kwani yu hoi kitandani akisumbuliwa na kichwa pamoja na mgongo.

 

Akizungumza na Za Motomoto News, Wastara alisema yupo kwenye mateso makubwa ya mau­mivu ya kichwa na mgongo na tarehe ya kurudi hospitali nch­ini India imeshafika lakini ameshindwa kwenda kutokana na kukosa fedha za matibabu.

 

“Dawa nime­maliza na muda wa kurudi hospitali umefika lakini sina fedha mpaka sasa, nimefuatilia fedha za kazi niliyofanya na Wahindi walioni­sainisha mkataba wa kuwa balozi wa simu zao lakini mpaka leo hawajanilipa cho­chote na wametoroka, nimechanganyikiwa tu hapa, namuomba Waziri Harrison Mwakyembe (Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo) anisaidie ili nipate haki yangu niweze kwenda kutibiwa,” alisema Wastara.

Comments are closed.