The House of Favourite Newspapers

Watano Wawekewa Pingamizi Simba

MAMBO yameendelea kuwa moto kuelekea uchaguzi mkuu wa Simba baada ya wagombea watano katika nafasi tofauti ku­wekewa mapingamizi.

 

Uchaguzi wa Simba unafanyika Novemba 3, kwa ajili ya kupata viongozi wapya watakaoiongoza Simba katika kipindi kijacho cha miaka minne baada ya wale wa awali kumaliza muda wake.

 

Zaidi ya wanachama 21, wamechukua fomu za kuwania uongozi katika nafasi mbalimbali ikiwemo ya uenyekiti ambao watachaguliwa kwa misingi ya katiba mpya ya klabu hiyo ya mwaka 2018, katika ibara ya 27 ambapo mwenyekiti lazima awe na shahada.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba, Boniface Lyamwile amesema; “Tunakwenda hatua kwa hatua na tayari kwa sasa tumefikia hatua ya mapingamizi na kuna wagombea watano ambao wamewekewa mapingamizi.”

 

“Tutawakutanisha wagombea wote waliowekewa mapingamizi na wale ambao wamewawekea mapingamizi wenzao ili kuweza kujadiliana juu ya kile kilicholetwa chini ya wanakamati wote kisha tutatoa maamuzi.

 

“Hakuna mtu ambaye ataonewa katika hili kila kitu kitakwenda sawa kwa mujibu wa sheria zetu tutatoa maamuzi kulingana na ukweli jambo,” alisema Lyamwile ingawa kamati ya uchaguzi ya TFF imesisitiza kuwa uchaguzi huo haupo kwavile kuna vitu vingi haviko sawa.

 

Comments are closed.