The House of Favourite Newspapers

WATANZANIA WATUNUKIWA WARSHA YA KUENEZA UMEME ITALIA

 WATANZANIA wawili wataalam katika mradi wa kueneza umeme vijijini wamepata tuzo kwenye Warsha ya Uwekezaji ya Umoja wa Kueneza Umeme Vijijini (ARE) kwenye kisiwa cha Sicily nchini iliyofanyika Italia Machi 13 hadi 18 mwaka huu.

 

Hiyo imetokea katika warsha hiyo iliyokutanisha wawakilishi kutoka taasisi zinazoendelea, sekta binafsi, mamlaka za fedha na teknolojia kutoka Afrika, Asia, Amerika ya Kusini na Ulaya kujadili mielekeo ya uenezaji wa viwanda, miundo ya sera za nishati na ujumuishaji wa nchi zinazoendelea katika kuinua uchumi kupitia mifumo ya uenezaji wa umeme vijijini.

Mfanyakazi wa shirika la uenezaji wa nishati ya jua nchini (ENSOL), Prosper Magali (katikati) akipokea tuzo.

Watanzania hao ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la uenezaji wa nishati ya jua nchini (ENSOL) Hamisi Mikate na Mkurugenzi wake, Prosper Magali.

 

Katika tukio hilo, washiriki walizungumzia kwa kirefu kujumuisha juhudi mbalimbali kwa ajili ya kutatua suala la umeme kwa kushirikiana na sekta za kilimo, maji na nishati.

 

Kikao hicho pia kilitambua kampuni na taasisi mbalimbali ambazo zimetoa mchango katika kuendeleza uenezaji wa umeme vijijini katika nchi zao.  Miongoni mwa taasisi hizo 17, miradi miwili kati yake ni ya Tanzania, ambayo ikawa washindi wa tuzo za ARE katika makundi yake.

 

Katika taarifa yake ya shukurani, Mkurugenzi na Mwasisi-Mwenza wa taasisi ya kueneza umeme katika Bonde la Ufa (RVE), Franz Kottulinsky, alisema:

 

“Nakumbuka miaka kadhaa tulivyoanzisha kampuni yetu, mradi wetu wa kwanza wa umeme wa kutumia maji ukiwa Nyanda za Juu Kusini Tanzania, hapakuwa na chochote bali mto uliokuwa ukitiririsha maji kimyakimya, umbali wa kilomita zipatazo 100 kutoka gridi y taifa ambapo katikati yake kulikuwa na vijiji 34 ambavyo havikuwa na umeme.

 

“Leo nikipita katika eneo hilo, ambako kuna njia za umeme zilizoenea katika urefu wa kilomita 300, ninashuhudia miradi mingi ya biashara ikiendelea katika maeneo ya Mufindi na Kihansi, yote ikitumia umeme na kuwawezesha watu kuishi maisha bora.”

Comments are closed.