The House of Favourite Newspapers

Watatu Wafariki na Maelfu Hatarini Kutokana na Kusitishwa kwa Misaada ya Chakula Sudani Kusini

0
Watoto wanaoishi katika mazingira magumu ya kukosa chakula kwenye makambi ya wakimbizi nchini Sudan Kusini

WATOTO wawili na mtu mzima mmoja wameripotiwa kufariki kutokana na njaa ikiwa ni baada ya Umoja wa Mataifa kupitia Programu ya Chakula Duniani (WFP) kutangaza kusitisha msaada wa chakula kwenye baadhi ya maeneo nchini Sudani ya Kusini kwa madai ya kukosa pesa.

 

Mnamo mwezi juni Shirika hilo lilidai kuwa lilikuwa linahitaji kiasi cha Zaidi yad ola milioni 426 ili liweze kusambaza vyakula kwa walengwa, lakini msaada huo haujapatikana kutokana na mashirika mengi ya kimataifa kutupia macho amajanga mengine ikiwemo lile la vita ya Ukraine na Urusi.

 

Sami Al Subaihi mmoja wa wafanyakazi kwenye makazi ya wakimbizi amedai kuwa moja yam toto aliyefariki kwa njaa alikuwa na umri wa miaka mitano tu.

Wakimbizi wakiwa katika kambi zao nchini Sudan Kusini

“Nilimuona mama mmoja akiwa na mtoto mwenye umri wa miaka 5 akiwa amekonda na akiwa amedhoofu, akawa anachimba kaburi.” Alisema Sami.

 

Ameendelea kusisitiza kuwa zaidi ya watu wengine 20,000 wanaoishi katika makambi maalum ya wakimbizi wapo katika hatari ya kufa kwa njaa kutokana na kukosekana kwa misaada ya chakula.

 

“Kwenye kambi moja nimeona watu wakidondoka wakiwa taabani, ni wazi kwamba hawajapata chakula kwa muda fulani sioni mtu yeyote akipika au kuwepo kwa chakula kilichohifadhiwa katika makazi yao.

Leave A Reply