The House of Favourite Newspapers

RC Makalla Akiri Athari za Madawa ya Kulevya ni Kubwa katika Jiji la Dar es Salaam

0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amekiri mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Jamhuri ya Muungano wea Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa athari za madawa ya kulevya katika mkoa wa Dar es Salaam ni kubwa sana.

 

RC Makalla ameyasema hayo katika hafla ya maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za kulevya Duniani ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

 

Aidha RC Makalla amegusia kuwa moja ya athari kubwa za madawa ya kulevya ni Pamoja na vijana wa Panya Road ambao amethibitisha kuwa kama Mkoa umefanikiwa kuwadhibiti kwa kiasi kikubwa ingawa chanzo cha vijana hao kufanya matukio ya uhalifu ni kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya ambayo ndiyo huwasukuma na kutekeleza matukio hayo ya uhalifu ikiwemo kukata watu kwa mapanga.

RC Makalla amebainisha kuwa athari za mawada ya kulevya mkoa wa Dar es Salaam ni makubwa

“Athari ni kubwa Mheshimiwa Waziri Mkuu ya madawa ya kulevya na hili linathibitishwa pia hata oparesheni ya Panya Road katika Mkoa wa Dar es Salaam nimefanikiwa vizuri lakini hatutaki kurudi huko, ukiwauliza wale Panya Road ukiwakamata wanakuambia hawezi kumpiga mtu panga au kumchoma kisu mpaka avute bangi ili kuondoa aibu sasa bangi ni madawa ya kulevya sasa vijana wanakuwa na tamaa ya kupata chochote kile wanakimbilia kwenye madawa ya kulevya na mwisho wa siku wanakuwa waalifu.” Amesema RC Makalla.

 

Kwa upande mwingine RC Makalla amesema kama Mkoa wamejipanga kushirikiana na mamlaka na taasisi mbalimbali kuhakikisha wanakomesha kabisa matumizi ya dawa za kulevya katika Mkoa wa Dar es Salaam na nchi nzima.

Leave A Reply