Wateja 15 waibuka kidedea Promosheni ya DStv ya Tia Kitu pata vituz!!

Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo akichezesha droo ya kupata washindi wa huku Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Humudi Semvua (kulia) akifuatilia kwa makini. Kushoto ni Benson Urio wa kitengo cha Teknohama cha DStv.

Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo (Katikati) Akizungumza kwa simu na moja ya washindi wa promosheni hiyo.

 

 

Ijumaa Machi 08, 2019. Hatimaye washindi 15 wa wiki ya pili ya promosheni ya “Tia kitu pata vituz” inayoendeshwa na MultiChoice Tanzania watangazwa chini ya usimamizi wa Afisa Mwandamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Bw. Humudi Semvua. . Kampeni hiyo itadumu kwa kipindi cha wiki 8, na itakuwa ikitoa washindi 15 kila wiki hivyo jumla ya washindi 120 katika kipindi chote cha promosheni hiyo.

 

 

Promosheni hiyo ni ya wazi kwa wateja wote wa DStv ambao watalipia vifurushi vyao kabla havijakatika. “Mteja yeyote wa DStv atakayelipia kifurushi chake kabla hakijakatika moja kwa moja anaingia katika droo na ana fursa ya kujishindia kifurushi chake kwa muda wa miezi miwili” alisema Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo wakati wa kufanya droo ya wiki ya pili ya promosheni hiyo.

 

 

Akizumgumza baada ya kupatiwa taarifa kuhusu ushindi wake huo Yohana Yunge ambaye ni mteja wa DStv aliyepo mkoani Mbeya amesema kuwa anafurahishwa na jitihada zinazofanywa na DStv siku kwa siku katika kuwajali na kuhakikisha wateja wake wanapata huduma zilizo ubora wa hali ya juu.

 

Naye bi. Saida Abdallah kutoka Kagera, ameishukuru sana DStv kwa zawadi hiyo na kueleza kuwa kweli DStv inawakumbuka wateja wake.

 

Toa comment