The House of Favourite Newspapers

Fundi Ujenzi mwingine ajishindia Sh Mil. 31.8 za SportPesa

MAFUNDI Ujenzi wamecharuka kushinda Jackpoti Bonasi ya SportPesa ni baada ya mwingine, Daniel Pius Lubigiri kujishindia Shilingi Milioni 31, 858, 827 baada kubashiri kwa usahihi mechi 12 kati ya 13.

 

Huyo fundi wa pili wa ujenzi kushinda ndani ya wiki moja baada ya juzi Juma Mililu wa Buza Kanisani jijini Dar es Salaam kujishindia kiasi hicho fedha baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 12 kati ya 13.

 

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar, Lubigiri alisema kuwa ushindi huo wa Jackpoti Bonasi umefanikisha malengo yake aliyoyaweka ya muda mrefu, hivyo ndoto zake zimetimia kwa kiasi kikubwa.

Lubigiri alisema, huyo ni ushindi wake wa kwanza kuupata tangu aanze kucheza na SportPesa kwa muda mfupi akiamini matatizo yake yatamalizika.

 

“Huu ni ushindi wangu kwanza tangu nimeanza kucheza kubashiri na SportPesa, kiukweli ninajisikia furaha baada ya ushindi huu wa fedha nyingi nilizoshinda.

 

“Niwatoe hofu watu wote wanaonifahamu waamini kuwa ni kweli mshindi anapatikana wa haki pale anaposhinda ubashiri wake kwa usahihi kama ilivyokuwa kwangu.

 

“Hivyo, baada ya ushindi huu malengo yangu yatakuwa yametimia kwa kiasi kikubwa kutokana na mipango niliyojiwekea,”alisema Lubigiri.

 

Kwa upande wa SportPesa, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni hiyo, Tarimba Abbas alimpongeza mshindi huyo huku akimtaka kuendelea kubashiri na SportPesa ili ajishindie Jackpoti ya Shilingi Milioni 500.

 

“SportPesa imepanga kuboresha maisha ya Watanzania kupitia ubashiri wao wa mechi, hivyo ni vema wakabashiri na SportPesa ili kufanikisha ndoto zao kwa kushinda fedha,”alisema Tarimba.

Comments are closed.