The House of Favourite Newspapers

Wateule Tuzo ya BBC kwa Mchezaji Bora Afrika 2018 Watangazwa

Image result for Medhi Benatia

Wachezaji wa soka barani Afrika walioorodheshwa kuwania tuzo ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kwa mwanasoka bora zaidi mwaka huu ni Medhi Benatia (Morocco), Kalidou Koulibaly (Senegal), Sadio Mane (Senegal), Thomas Partey (Ghana) na Mohamed Salah (Misri). 

Upigaji kura ulianza jana (Jumamosi) rasmi Novemba 17 saa nne usiku kwa saa ya Afrika Mashariki na utakamilika mwezi Desemba 2, mwaka huu saa tano usiku. Mshindi wa tuzo hiyo atatangazwa katika kipindi cha BBC World News Desemba 14 mwaka huu saa mbili  na nusu kwa saa ya Afrika Mashariki.

Orodha ya waliyoteuliwa imeandaliwa na jopo la wataalamu wa kandanda barani Afrika. Mshambuliaji wa Liverpool Salah ndiye aliyeshinda tuzo ya mwaka jana. Wachezaji wengine waliowahi kushinda tuzo hiyo ni pamoja na Jay-Jay Okocha, Michael Essien, Didier Drogba, Yaya Toure na Riyad Mahrez.

Related image

Beki wa kati wa Juventus Benatia, 31, ameshinda ligi mara nne mfululizo mwaka huu – mbili kati hizo akiwa na Bayern Munich na mbili zingine akiwa Juve. Pia alikuwa nahodha wa Morocco katika michuano ya Kombe la Dunia ya msimu wa joto mwaka huu.

Mlinzi wa Napoli Koulibaly, 27, aliiwakilisha katika klabu hiyo kuchuana dhidi Juve katika kinyang’anyiro cha fainali ya ligi ya Serie A ya Italia ikiwa ni pamoja na ushindi maarufu dhidi ya miamba hao wa ligi ya mabingwa.

Image result for Sadio Mane

Sadio Mane, aliichezea Senegal dakika zote 270 katika michuano ya Kombe la Dunia. Mshambuliaji  huyo wa Liverpool mwenye umri wa miaka 26, pia aliiongoza nchi yake  kuishinda Japan. Alikuwa mfungaji bora wa pili katika ligi ya mabingwa wa Ulaya msimu uliyopita — aliifungia Liverpool mabao 10, ikiwa ni pamoja na bao moja aliyoifungia walipochapwa 3-1 na Real Madrid katika fainali.Related image

Kiungo wa kati wa Atletico Madrid Partey, 25,alichaguliwa kuwa katika kikosi cha kwanza cha Diego Simeone baada ya kuonyesha umahiri ikiwa ni pamoja na kuwa mchezaji wa ziada katika fainali ya ligi ambapo waliishinda Marseille.Image result for mo salah

Mshambualiaji wa Liverpool Salah, 26, alishinda taji la mfungaji wa mabao mengi zaidi (32) katika ligi kuu ya England mwezi Mei.  Sawa na Mane, alifunga mabao 10 katika ligi ya mabingwa kuelekea fainali. Aliifungia Misri mabao yote ya kombe la Dunia.

Comments are closed.