The House of Favourite Newspapers

HUKU AKITANGAZA KUPORA MUME WA MTU UWOYA AZUA TAHARUKI

BAADA ya kutangaza kuwa anataka kukwapua bwana wa mtu, staa wa Bongo Movies, Irene Uwoya, amezua hofu ya aina yake kwa mastaa wenzake ambao wamekuwa wakiwategemea mabwana zao kwa kila kitu mjini.  Kupitia ukurasa wake wa Instagram, juzikati aliweka picha yake na kusindikiza na ujumbe kwa lugha ya Kingereza uliosomeka hivi:

“Father! Forgive me for I’m about to steal someone’s boyfriend… because when they stole mine you didn’t say anything!” Akiwa na maana kwamba, asamehewe anakwenda kuchukua bwana wa mtu kwani yeye alipochukuliwa bwana wake, hakuna aliyesema kitu kumtetea.

Baada ya kuandika maneno hayo, mastaa wa wakubwa wa kike wawili walioomba hifadhi ya majina yao ambao walizungumza na Risasi Jumamosi, walieleza kuwa na hofu na Uwoya kwa kile walichosema kuwa mrembo huyo hana masihara.

“Wewe Uwoya unamjua unamsikia. Sasa hivi hana bwana, anaweza kufanya kweli yule kwa kweli ametutia hofu na hali yenyewe hii ya sasa hivi kama unavyoijua, ukishikwa na mtu inabidi kumlinda kwelikweli asije akanyakuliwa,” alisema msanii huyo.

Mwingine naye alisema:

“Sisi mastaa tunajuana, Uwoya kweli akimtaka bwana wako hamkosi. Atafanya kila linalowezekana na kweli utasikia ametoka naye.” Mbali na mastaa hao, Risasi Jumamosi lilielezwa na watu wa karibu na mastaa wengi wa kike kuwa wamekuwa na hofu baada na kauli ya Uwoya kwani uzuri wa umbo lake ni silaha tosha ya kuwaingiza ‘kingi’ waume wa mastaa.

Baada ya kuzungumza na vyanzo mbalimbali kuhusu kauli hiyo ya Uwoya, Risasi Jumamosi lilimvutia mrembo huyo ili kujua ni nini kiini cha yeye kusema maneno hayo na juu ya hofu aliyoiibua kwa mastaa wenzake ambapo alipopatikana alisema anashangazwa na watu ambao wanaihofia kauli yake.

Alisema, ni msemo wake ila pamoja na hilo, kweli anatarajia kuibuka na bwana wake mpya atakayewashangaza wengi. “Mimi najua kila mtu yuko katika tumbo joto lakini pia sijui kwa nini wanaogopa wangejikaza tu hivyohivyo watamuona mtu ambaye atakuwa wangu sasa na nitawashangaza watu wengi sana,” alisema Uwoya.

Uwoya amedaiwa kumwagana na mume wake ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ kwa madai msanii huyo amekuwa akichepuka nje ndoa.

STORI: Imelda Mtema, Risasi Jumamosi

Comments are closed.